Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFUASI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameonywa wasikubali kulipiwa
ada za uanachama na baadhi ya wanasiasa wenye lengo la kugombea nafasi
mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu, badala yake walipe wenyewe.
Baadhi ya wanasiasa wenye lengo la kugombea kwenye chaguzi zijazo
wanatuhumiwa kuwalipia ada wanachama wenye madeni ili wawapigie kura.
Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha
Mjini, Mwenyekiti wa chama hicho Tumbi, Charles Kapama, alisema baadhi
ya wanachama wanalipiwa ada na wenzao wanaotarajia kugombea uongozi
kwenye chaguzi zijazo.
“Kila mwanachama anatakiwa alipe kadi yake badala ya kulipiwa na mtu
ama watu… kufanya hivyo ni kukiuka taratibu, miongozo na kanuni za
chama, kumbukeni ukilipiwa na wewe lazima ulipe fadhila kwa kumchagua
mtu huyo hata kama hafai,” alisema Kapama.
Alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji, wenyeviti wa vijiji na
serikali za mitaa kuitisha mikutano kwenye maeneo yao kwa ajili ya
kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao.
Mwenyekiti huyo alisema baadhi ya viongozi hao hawaitishi mikutano
hiyo hali inayosababisha wananchi kuamini kwamba kuna matumizi mabaya
ya fedha zao yanayofanywa na viongozi waliopo madarakani
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment