Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATUMISHI wa Huduma ya Afya watakaogundulika kutoa huduma za
ubaguzi kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) taarifa
zao zitafikishwa wizarani, ili waweze kuchukuliwa hatua.
Baadhi ya watumishi katika idara ya afya wamekuwa wakilalamikiwa na
wanachama wa mfuko huo kutoa huduma kwa ubaguzi kwa kuwathamini zaidi
wagonjwa wanaotoa fedha papo papo.
Akizungumza mjini Kibaha hivi karibuni, Meneja NHIF Mkoa wa Pwani,
Andrew Mwilungu, alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa
wanachama wao na kwa sasa wanayafanyia kazi kwa kuwawajibisha
watumishi wenye tabia hiyo, kwani imekuwa ikichangia baadhi ya wananchi
kushindwa kujiunga na mfuko huo.
Mwilungu alisema kwa sasa wananchi wamekuwa wakihamasishwa kujiunga
na mfuko huo, hivyo wako kwenye mkakati wa kurekebisha mapungufu
yaliyopo kwa watoa huduma hao ambao wanatakiwa kubadilika na
kuwathamini wanachama wa mfuko huo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment