Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Mkoa (RC) wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ameiomba Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwasiliana na wamiliki wa vyombo vya
habari, hasa luninga, ili kuweka mkalimani wa lugha ya alama katika
taarifa za habari na vipindi maalumu.
Mahiza alisema uwepo wa mkalimani utawapa fursa watu wenye ulemavu wa
kusikia (viziwi) kuelewa na kufuatilia kinachotangazwa.
Akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na TCRA
wakiishirikisha Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi (TAMAVITA), alisema
kukosekana kwa mkalimani ni changamoto kwa viziwi.
Kwa upande wao, washiriki kutoka wilaya za mkoani Pwani, waliomba pia
kuwepo na mkalimani kwani wanakabiliana na changamoto hiyo, pia
wanapotumia mitandao ya simu za mkononi.
Ofisa Mkuu Masuala ya Mawasiliano wa TCRA, Thadayo Ringo, alisema
wamepokea maoni yao na kuahidi kuyafanyia kazi ili kundi hilo lipate
fursa ya kujua kinachotangazwa na kupata habari sawa na wengine.
Chanzo;Tanznia Daima
0 comments:
Post a Comment