Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI na wadau mbalimbali wameshauriwa kufanya kampeni za wazi
katika kukabiliana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi kwa
wanawake.
Mratibu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Uzazi
kilichoko hospitali ya Tumbi, Dk Alphonce Moyo, alisema jana kuwa
inatakiwa kuwekwa mipango mahususi ya kuhakikisha wanawake wanapata
elimu sahihi juu ya ugonjwa huo, ili wajitokeze kufanyiwa uchunguzi.
Moyo alisema endapo wanawake watapata elimu watahamasika kujitokeza
kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ambao kwa asilimia 90 unasaidia
kumaliza tatizo la saratani ya kizazi kwa wanawake.
Alisema serikali imeelekeza nguvu kubwa katika kupunguza vifo vya
wanawake wakati wa kujifungua, hivyo ni busara sasa kuwepo mikakati ya
kuwanusuru wanawake hao na saratani hiyo ambayo ni tatizo kubwa nchini.
Aidha, alisema tangu kitengo hicho kianzishwe mwaka 2011, wanawake
1500 wamechunguzwa na waliogundulika kuwa na saratani ya awali ni
wanawake zaidi ya 50 ambao walipatiwa matibabu ya awali.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment