Viongozi
mbalimbali wa Serikali akiwemo Mhe. Juma Nkamia (Naibu Waziri wa Habari
na Michezo), Mhe. Jenista Mhagama (Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi), Mhe. Halima Mdee (Mbunge wa Kawe), Mhe. Martha Mlata (Mbunge
Viti Maalum) wametokea katika video ya pamoja wakiunga mkono na
kupongeza mashindano ya Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula
yanayoendelea hivi sasa.
"Ukichukua
mazingira ambayo wakina mama wengi wanaishi, vijana wengi wanayoishi,
wakati mwingine unaona kwamba wanapoteza mwelekeo, lakini wanapopata
nafasi ya kushiriki, kwa mfano kwenye Maisha Plus, wanapata pia nafasi
nyingine ya kujifunza mambo mapya na utamaduni halisi wa taifa letu la
kitanzania." Anasikika Mhe. Jenista Mhagama.
Mashindano
hayo ambayo yanafanyika katika kijiji cha siri cha Maisha Plus
yanawakutanisha wakulima wanawake wapatao 20 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania pamoja na vijana 16 walioingia fainali kutoka nchi za Burundi,
Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda.
Fainali
za mashindano hayo zinatarajiwa kufanyika tarehe 18/05/2014 ambapo
mshindi kwa upande wa Mama Shujaa wa Chakula atajishindia zawadi ya
vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 25 (Milioni 5 katika
hizi ziliongezwa na Mhe. Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi siku alipowakaribisha Mama Shujaa kijijini INGIA HAPA KUONA TUKIO LA AWALI LA UZINDUZI na mshindi kwa upande wa vijana atajishindia Tzshs. Milioni 25 ya mradi atakaopendekeza.
Fainali hizi zitaonyeshwa LIVE na TBC1 siku ya Jumapili tarehe 18/05/2014 kuanzia saa nne usiku.
MAISHA PLUS/MAISHA SHUJAA WA CHAKULA
MAISHA PLUS/MAISHA SHUJAA WA CHAKULA

0 comments:
Post a Comment