Home » » MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS, PROFESA ANNA TIBAIJUKA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO.

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS, PROFESA ANNA TIBAIJUKA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi akisalimiana na akina Mama Shujaa wa Chakula ambapo jana ndio waliingia Rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus
Mama Shujaa wa Chakula wakipunga mkono kuwakaribisha wageni waalikwa
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa Chakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.
Balozi wa OXFAM Tanzania Khadija Mwanamboka akizungumza jambo wakati wa Sherehe za kuwakalibisha Mama shujaa wa Chakula katika kijiji cha Maisha Plus.



Hawa ndio Mmaa Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi  wa pili kulia, akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi pamoja na wageni wengine wa meza kuu wakitazama Taarifa Mbalimbali za Mama shujaa wa Chakula katika Runinga ambayo haipo Pichani.
Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Muwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi  ili aweze kutoa hotuba yake
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula, Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014
Mmoja wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
Washiriki wa Maisha Plus kikaangoni
Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana

Picha ya Pamoja Mgeni   Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi, Wakina Mama Shujaa wa Chakula, Vijana wa Maisha Plus pamoja na wadau mbalimbali waliofika katika sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula  Kijiji cha maisha Plus

Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijiji hicho
Mama  Shujaa wa Chakula wakipata maelekezo Mbalimbali juu ya Kijiji Hicho
Moja ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus
Mama Shujaa wa Chakula pamoja na Vijana wa Maisha Plus wakifurahia baada ya kuungana kijijini hapo
Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa