Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),
inatarajia kuanza utaratibu wa kutoa vibali maalumu vitakavyolenga
kumuwajibisha dereva au kondakta moja kwa moja badala ya mmiliki kama
ilivyokuwa awali, lengo likiwa ni kudhibiti makosa ya barabarani.
Ofisa Mkuu wa Sumatra Mkoa wa Pwani, Iroga Nashon, alieleza hayo juzi
alipozungumza na waandishi wa habari. Kwamba mamlaka hiyo imefikia
hatua hiyo baada ya baadhi ya madereva kurudia makosa mara kwa mara,
hata baada ya kutozwa faini.
Alisema awali kosa lolote ilimbidi mmiliki kuwajibika ikiwemo kutozwa
faini ambayo huanzia sh 250,000. Lakini kwa sasa itamlazimu dereva ama
kondakta kuwajibishwa moja kwa moja ili kuwawezesha waheshimu sheria
zilizowekwa.
Nashon alisema vibali hivyo pia vinalenga kuwarekebisha na endapo
dereva au kondakta atakutwa na kosa atanyang’anywa kibali na kuzuiliwa
kazi hadi atakapojirekebisha.
Alisema mpango huo wa kitaifa upo kwenye hatua za awali na unatarajiwa kuanza kutumika baada ya mwaka wa fedha ujao.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment