Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mratibu wa shindano hilo,
Teddy Chilala, alisema kwa sasa tayari warembo wanane wameshaanza
kujinoa vilivyo katika Ukumbi wa Blue Nile na kuwa maandalizi yote
yanakwenda vizuri.
Mratibu huyo alibainisha kuwa shindano hilo litapambwa na burudani
mbalimbali za muziki wa dansi hapa nchini, ikiongozwa na bendi ya JKT
Ruvu chini ya kiongozi wao mpya, Hamis Kayumbu ‘Amigolas’ pamoja na
Mhina Panduka ‘Toto Tundu’.
Aliongeza kuwa shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake, kutokana
na kuwashirikisha warembo ambao ni wazawa wa Wilaya ya Kibaha na kutoa
wito kwa wakazi wa mji huo na maeneo mengine ya jirani, kujitokeza kwa
wingi kwenda kushuhudia onyesho hilo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment