Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa CCM, Tawi la Lumumba katika Kijiji cha Kilimani
Mashariki kilichopo Kata ya Ngorongo, Rufiji, Saidi Simba (60),
amefariki dunia kwa kuliwa na mamba baada ya kuzama na mtumbwi alipokuwa
akienda shambani.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kilimani Mashariki,
Masudi Mminge alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Mto Rufiji wakati
mwenyekiti huyo alipokuwa akivuka kwenda ng’ambo ya pili kwa ajili ya
kilimo.
Mminge alisema jitihada za kumtafuta zimekwama
kutokana na eneo hilo kuwa na mamba wakubwa hivyo kuwafanya wananchi
kuwa na hofu ya kuliwa.
Alisema kila walipokuwa wakifika sehemu za vichaka
vya mto walikuwa wakisikia harufu kali lakini juzi harufu hiyo
ilitoweka jambo ambalo limewafanya waamini kuwa ndugu yao ameshakufa na
ameliwa na mamba.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment