Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantumu Mahiza
Mbali na nyumba kuharibika na watu kukosa makazi, pia daraja ambalo ni kiungo cha vijiji vya Muhoro, nalo limezama na kusababisha watu kutumia boti kuvushwa kwenda upande wa pili.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Khatibu Chaulembo, aliliambia NIPASHE jana kwamba mafuriko hayo yalianza toka mwishoni mwa mwezi uliopita na watu wanne kufariki dunia siku tatu zilizopita.
“Haya mafuriko yameleta athari kubwa na bado yanazidi kuwa makubwa na hali hiyo imeilazimisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa kufika katika eneo la matukio ili kujionea hali ilivyo na kuipatia jamii taarifa ya kila wanachokiona katika mafuriko haya,” alisema Chaulembo.
Aliongeza kuwa kutokana na mafuriko hayo kuwaathiri wakulima, halmashauri imeshaomba tani 874 za chakula kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa.
Alisema kuwa chakula hicho kitatumika kwa mwezi mmoja kwa ajili ya waathirika hao.
Alisema pia halmashauri imetoa boti mbili kwa ajili ya kuwabeba wananchi wanaokwenda maeneo ya Muhoro mjini au vijiJini.
“Watu wote wanaosafiri kutoa Jiji la Dar es Salaam kwenda Muhoro wanalazimika kuishia njiani kutokana na kuzama kwa daraja la Muhoro ambalo linaunganisha vijiji vyake, lakini halmashauri imetoa boti mbili ambazo watu hujitolea mafuta ili kuwekwa katika hizo boti na kuvusha watu,’’ alisema Chaulembo.
Katika hatua nyingine, Chaulembo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, amewaagiza madiwani wote wa halmashauri hiyo kwenda katika maeneo yao ili wawe wanatoa taarifa za mafuriko na hatua zinazochukuliwa.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment