Maisha ya wanakijiji cha
Maisha Plus yameendelea kuwa mazuri siku hadi siku. Kazi ziliendelea kama
kawaida huku wanakijiji wakijadili na kutafakari toka walipowasili kijijini
hapo mpaka sasa. Wanakijiji wengi walikuwa na mtazamo tofauti walipoingia tu
kijijini na kudhani kuwa watashughulika na kilimo pekee. Hali imekuwa tofauti
kwani wanakijiji wameweza kujifunza mambo mbalimbali mazuri na yenye manufaa
kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla punde watakapo rudi. Uzoefu walioupata
mpaka sasa ni pamoja na utengenezaji wa batiki, sabuni ya maji na kibande,
mafuta mazito ya kujipaka, utengenezaji wa jiko la gesi, jiko linalotunza joto,
ufugaji bora wa kuku bila kusahau kilimo hai.
Pamoja na hayo baadhi ya
vijana wa kijiji cha Maisha Plus kwa siku ya leo walikwenda porini kwa lengo la
kuweka mitego ya kutega ndege aina ya kanga na samaki katika bwawa lililopo
jirani na kijiji hicho. Vijana hawa wamefanya hivyo kama mchango wao kusaidia
familia zao kupata kitoweo japo hawakuweza kupata chochote kwa siku hiyo na
kurudi nyumbani mikono mitupu.
Kwa kuwa wanakijiji walikosa
fursa ya kuchukua ufunguo uliopo kwa chatu na kufungua boksi lililo na fedha taslimu kiasi cha
shilingi 300,000 wanakijiji hao walipewa swali ambalo halikuweza kurudiwa na
muulizaji na haikuruhusiwa kuuliza maswali kama masharti ya swali hilo ili
kuwaachia wanakijiji hao kazi ya kutafakari na kufanya kile walichoagizwa.
Swali hilo lilikuwa linasema hivi ‘tengeneza system yenye mfumo wa mchanganyiko
wa hydrotherapy na liquid therapy bila kuhusisha maji kwa ajili ya kupunguza
magonjwa ya kuharisha kwa watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka mitano’
je, swali la kujiuliza wanakijiji cha Maisha Plus wataweza kutengua kitendawili
hicho? Tuone kipindi kijacho kwani wanakijiji hicho walikuwa bado wanajadili
nini cha kufanya.
0 comments:
Post a Comment