Home » » CHUMBA CHA MAITI TUMBI CHAFUNGULIWA

CHUMBA CHA MAITI TUMBI CHAFUNGULIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid
 
Huduma ya kuhifadhi maiti  katika Hospitali teule ya Rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi imerejea baada ya Serikali kutoa jokofu lenye uwezo wa kuhifadhi miili 16.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Bryson Lothi, alisema kurejea kwa huduma hiyo itarahisisha uhifadhi wa miili ya watu wanaofariki kupata sehemu salama za kusubiria taratibu za mazishi.

 Lothi alisema awali wakati mashine hiyo haijafika huduma za kuhifadhi maiti ilikuwa ikitolewa kwa taabu kwa sababu miili ilikuwa inaharibika na kukwamisha wafiwa kusubiri taratibu za mazishi, hivyo ndugu walilazimika kuhamishia miili ya jamaa zao katika hospitali zingine za jirani zikiwamo Amana, Temeke na Muhimbili hatua ambayo mbali na usumbufu pia iliongeza gharama kwao.

 Hata hivyo, alisema mbali na kupatikana mashine hiyo mpya, lakini bado inahitajika nyingine ili kukidhi mahitaji kwani Hospitali ya Tumbi wakati mwingine huelemewa na miili ya marehemu kutokana mara nyingi kupokea miili mingi kutoka nje inayopelekwa na Polisi kwa ajili ya kusubiri ndugu.

Mingine ni inayotokana na ajali za magari katika barabara kuu ya Morogoro- Chalinze na Chalinze-Segera.
 Mwishoni mwa mwaka jana,  uongozi wa hospitali hiyo uliamua kufunga chumba cha kuhifadhia maiti kutokana na mashine zake zote mbili za kupoozea kuharibika na kushindwa kupooza miili.

Kutokana na hatua hiyo, maiti wote waliokuwa wanafia wodini hospitali hapo ama wale wanaofia nje walilazimika kupekelekwa kuhifadhiwa katika hospitali za jijini Dar es Salaam.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa