Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ukosefu wa kituo hicho umekuwa ukisababisha damu inayokusanywa
hospitalini hapo kutotumika hadi pale itakapopelekwa makao makuu ya damu
salama kupimwa na baadae kugawanywa kwenye hospitali na vituo vya afya.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hospitali hiyo kujua
changamoto zinazoikabili, Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk.
Brayson Kiwelu, aliomba wafadhili kujitokeza kusaidia ujenzi wa kituo
hicho, ili damu inayokusanywa iweze kutumika kwa wagonjwa wa hospitali
hiyo.
Alisema endapo kituo hicho kitajengwa kitasaidia kuondoa upungufu wa
damu katika hospitali hiyo pamoja na watu wengi kujitokeza kuchangia
damu.
“Hospitali yetu imekuwa ikikusanya damu nyingi, lakini kutokana na
kutokuwa na kituo damu hiyo imekuwa ikienda kupimwa makao makuu na
baadae tunapata mgawo kama hospitali nyingine ambao damu hiyo haikidhi,”
alisema Dk. Kiwelu.
Hospitali hiyo pia inakabiliwa na upungufu wa madaktari ambapo kwa sasa wapo 11 huku wanne kati yao wakiwa masomoni.
Pia Dk. Kiwelu ameiomba serikali kusaidia fedha kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya hospitali hiyo kutokana na mengi kuchakaa.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment