Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI wa Kijiji cha Dihozile, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wanatembea kwa saa mbili kufuata huduma ya maji ya malambo.
Wakizungumza na Tanzania Daima hivi karibuni, walisema tangu kijiji
hicho kianzishwe hawajawahi kupata huduma ya maji, hivyo kulazimika
kutumia maji ya malambo.
Mwajuma Hamis, mkazi wa Dihozile, aliiomba serikali kuingilia kati
kusaidia upatikanaji wa maji katika kijiji chao ili kuondokana na adha
ya kutumia muda mwingi kufuata huduma hiyo.
Mwajuma alisema baadhi ya shughuli za kimaendeleo zinashindwa
kufanyika kwa wakati kutokana na ukosefu wa maji ya uhakika katika eneo
hilo.
Nao wakazi wa Kijiji cha Saadani Chumvi wilayani hapa, wanakabiliwa
na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama, na hivyo kulazimika
kutumia maji ya malambo ambayo hutumiwa pia na wanyama waliopo kwenye
hifadhi.
Hadija Juma, mkazi wa kijiji hicho, ameiomba serikali kuwasaidia
kuwafikishia huduma ya maji katika eneo lao kwani kwa sasa wako katika
hali mbaya ya kutumia maji na wanyama ambayo yamekuwa yakiwasababishia
homa za matumbo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment