JESHI la polisi mkoani Pwani linamshikilia Daud Ramadhani (21) kwa kosa la kujifanya askari polisi.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Disemba 29 saa nne usiku katika eneo la
Kwamatiasi kata ya Mkuza wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, baada ya jeshi
la Polisi kupata taarifa kutoka kwa wananchi zilizodai kuwepo kwa mtu
anayejifanya askari.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulricha Matei alisema baada ya kupata
taarifa hizo waliandaa mtego ambao juzi wakafanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo akiwa na kitambulisho bandia cha polisi, jozi moja ya
sare polisi jozi tatu za viatu vya Polisi.
Vitu vingine alivyokutwa navyo kwa ajili ya shughuli zake za kipolisi
ni pamoja na mikanda miwili ya kiunoni, kofia moja aina ya Balet pamoja
na mkanda wa filimbi.
Matei aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na kitambulisho chenye
namba H,136,2 Police kikiwa na majina ya Daud Ramadhani Iddi.
Alisema uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment