WATOTO wengi walio shuleni hawana elimu ya uzazi hali inayochangia ongezeko la mimba shuleni.
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Pre mature
Mothers Organization (TPMO), Konsolata Kayaga, alisema hayo mjini hapa
jana na kuongeza kuwa wameamua kutoa elimu ya mimba za utotoni ili
kupunguza tatizo hilo ambalo linachangia kudumaza maendeleo kwa ajamii.
Kayaga alisema kwa sasa wameanza kutoa elimu hiyo kwa watoto yatima wa
kituo cha Buloma kilichoko Kibaha, Pwani, ili kuwasaidia kujikinga na
maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) pamoja na mimba za utotoni.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watoto hususan wa kike
kutambua kuwa mimba za utotoni ni hatari kwa maisha yao, kwani mara
nyingi zimekuwa zikisababisha vifo.
Alisema ili kuweza kufikia malengo ni vema jamii ikashirikiana kupiga
vita mimba za utotoni ambapo kufanya hivyo kutakuwa njia sahihi ya
kuokoa maisha ya watoto wa kike.
Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Kibaha, Anatory Mhango, alivitaka vituo vya
kulelea watoto yatima kuhakikisha vinatoa elimu na maadili mazuri kwa
watoto hao, ili waweze kupunguza uhalifu na hatimaye waepuke vishawishi
vya wanaume wakiwa shuleni.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment