Home » » POLISI PWANI YATUNUKU NISHANI MAOFISA WA JESHI HILO

POLISI PWANI YATUNUKU NISHANI MAOFISA WA JESHI HILO

Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani limewatunukia nishani maofisa wa Jeshi hilo na baadhi ya wadau ambao wamelitumikia kwa uaminifu mkubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,Kamishna msaidizi mwandamizi ULRICH MATEI amesema kuwa hatua ya kuwatunukia nishani hizo maofisa na wadau ili kujenga utamaduni wa kupongezana na kutiana moyo. Kamanda MATEI amebainisha kuwa kuna changamoto mbalimbali katika suala zima la ulinzi na usalama, na amewataka watanzania kuhakikisha wanapanda mbegu za kuheshimu sheria bila shuruti kuanzia nyumbani ili kujenga jamii yenye kuzingatia maadili na utu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa