Home »
» PAC yasema lazima vyama vikaguliwe
PAC yasema lazima vyama vikaguliwe
|
|
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Deo
Filikunjombe, amesema ni lazima vyama vya siasa vifanyiwe ukaguzi kwa
kuwa vinapokea fedha za umma.
Hayo aliyasema juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajumbe wa
Kamati ya PAC na ile ya Serikali za Mitaa (LAAC) iliyofanyika Bagamoyo,
Pwani.
Filikunjombe alisema baadhi ya vyama vya siasa vinailalamikia kamati
yake kutoa taarifa ya kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali
(CAG), Ludovick Utouh kuvikagua vyama hivyo.
Alisema iwapo kuna vyama visivyopendezwa na suala hilo, vinatakiwa kuacha kupokea fedha za umma ili visikaguliwe.
Makamu huyo alisema tangu PAC iagize suala hilo, imejenga chuki kwa
baadhi ya viongozi wa vyama huku akisisitiza kwamba hadi Januari
mwakani kamati itaviita vyama vyote na kuvihoji ili kujua fedha za umma
zilivyotumika.
Filikunjombe alisema hadi sasa ni vyama vinne vilivyokabidhi ripoti
zao katika ofisi ya CAG ambavyo ni CUF, TLP, CCM na NCCR-Mageuzi.
Chanzo;Tanzania Daima
|
|
0 comments:
Post a Comment