Naibu Waziri wa Chakula Kilimo na Ushirika,Adam Malima
Aliyasema hayo juzi, katika Kikao cha Baraza la Madiwani, baada ya diwani wa kata ya Mkamba (CCM), Hassan Dunda, kuliambia baraza kuwa anashangaa kuona katika vitabu kuwa shule ya sekondari katika kaya yake imepatiwa madawati, meza na viti vya walimu, wakati taarifa hiyo siyo sahihi kutokana na yeye, kuwa na barua ambazo zinatoka kwa walimu zikidai shule hiyo haina vitu hivyo, ingawa afisa kutoka Mfuko wa Maendeleo (Tasaf), alitoa taarifa ya kutolewa vitu hivyo.
Malima ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo, alisema tatizo lililopo katika halmashauri hiyo ni watendaji kutokuwa karibu na madiwani na hali hiyo inasababisha madiwani kupata wakati mgumu pale wanapoulizwa maswali na wananchi.
"Sasa mtu anasema kapeleka madawati, viti na meza, wakati diwani wa eneo hilo, hana hata taarifa, sasa hamuoni kama hilo ni tatizo, na hivyo vitu vimepelekwa wapi, inatakiwa watendaji mnapokuwa na kitu cha kupeleka katika kata mjenge utaratibu wa kuwashirikisha madiwani ili kuepuka kama haya yasije kujitokeza tena,'' alisema.
Aliongeza kuwa, pia watendaji wamekuwa hawana taarifa sahihi za kata kutokana na kufanya kazi bila ya kuwashirikisha madiwani na hali hiyo inasababisha madiwani kupata maswali mengi ya kujibu kutoka kwa wananchi.
Aliahidi kufanya ziara ya kuibua kero za wananchi wiki ijayo kwa kutembelea kata 10.
"Tutasikiliza kero za wananchi, kwa mfano watazungumzia suala la maji, basi itabidi injinia ajibu jinsi atakapoweza kuzitatua, kufanya hivyo kuongozana na watu hao ni kutaka kuona jinsi watakavyoweza kuzisikiliza kero zao na kutoa majibu jinsi ya kuzitatua,''alisema.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment