SHIRIKA
la nyumba nchini limeipiga jeki ya sh. Milioni 10 shule ya sekondari ya
wavulana ya Marian wilayani Bagamoyo kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa jengo
moja la ghorofa tano ambapo itakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu itatoa fursa
ya vijana wengi wa kidato cha kwanza na tano wanaokosa nafasi kupata madarasa
ya kusomea mwakani.
Mbali
na kutoa fedha hizo, pia shirika hilo kupitia kwa Mkurugenzi wake mkuu Nehemia
Msechu jana limewahamasisha wazazi na walezi kuchangia ujenzi huo ambapo katika
harambee ya papo kwa papo zilipatikana sh.Milioni nane na mifuko ya saruji 300.
Akizungumza
na wazazi na walezi wa watoto wanaosoma kwenye shule hiyo huko wilayani
Bagamoyo, Msechu amesema ni vema jamii ikajenga tabia ya kuchangia katika
shughuli za maendeleo na siyo kwenye harusi,ngoma na kipaimara pekee
Msechu
amesema uridhi wa vijana katika wakati huu wa utandawazi ni elimu na si mali
wala fedha hata kama mzazi wake ni tajiri kiasi gani asipokuwa na utaalamu wa
kielimu hakuna chochote atakachokiweza kukimudu kuboresha maisha yake katika
suala Zima la maendeleo.-
Mkurugenzi
huyo wa shirika la nyumba la Taifa pia amewaasa wanafunzi wanaohitimu
kidato cha nne kuwa makini na kufuata maadili mema wanayofundishwa shulen,na
watambue ipo changamoto ya dawa za kulevya nchini tatizo ambalo wanapaswa
wajiandae kiakili na kimwili kwenda kukabiliana nalo huko mitaani watakapokuwa
baada ya kihitimu elimu yao.
Awali
wanafunzi 110 wanaohitimu kidato cha nne katika sekondari hiyo walimueleza
Msechu kuwa kutokana na elimu bora inayotolewa shuleni hapo kumekuwepo na
changamoto ya wazazi wengi kupeleka watoto wao hapo lakini kutokana na uhaba wa
madarasa imekuwa vigumu kuchukuliwa wengi hali ambayo imekuwa ikileta
malalamiko ya kunyimwa nafasi kumbe miundombinu ni chache
katika
risala yao iliyosomwa na Yusuf Omar wahitimu hao wamesema wao kama mabalozi wa
elimu ili kukabiliana na changamoto hiyo wamechangia mifuko 150 ya saruji ili
kuharakisha ujenzi wa madarasa unaoendelea na kuweza kuongeza idadi ya vijana
hapo mwakani,pia walitoa changamoto kwa wadau wa elimu nchin kuongeza maabara
zenye uwezo wa vitabu na vifaa vya kisasa ili kuzalisha wahitimu wanasayansi
halisi.
0 comments:
Post a Comment