Waamuzi wa mchezo wa
soka Mkoa wa Pwani wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa kufuata misingi ya haki
ili kuwezesha timu zetu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali
yanayohusiana na mchezo wa soka nchini.
Akizungumza katika
ufungaji wa mafunzo ya marefa Katibu wa Chama cha Marefa Tanzania,
BW.CHARLES NDAGALA amewapongeza marefa hao kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa
Pwani kwa kujitolea kifedha na kuweza kuhudhuria mafunzo hayo.
BW.NDAGALA
amebainisha kuwa anawashukuru Chama Cha Soka katika Mkoa wa Pwani, Kwa kuweza
kuchangia gharama mbalimbali kuwezesha kufanyika kwa semina hiyo kwa lengo la kuwapiga
msasa waamuzi hao ili waweze kufanya kazi yao kwa weledi.
Naye mgeni rasmi
katika ufungaji wa mashindano hayo, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya
COREFA, GODFREY NYANGE KABURU amewataka waamuzi hao kuzingatia misingi ya haki
wanapotekeleza majukumu yao, na hasa kutokana na klabu kutumia fedhaa nyingi
kuandaa mashindano.
NYANGE amewaeleza
waamuzi hao kuwa mashindano hayo yatawasaidia kufanya maamuzi sahihi
wanapokuwa wanachezesha mashindano mbalimbali na hivyo kusaidia kukuza kiwango
cha mchezo huo nchini.
0 comments:
Post a Comment