RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa atafurahi iwapo
kiwanda cha kuzalisha dawa za kuulia viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria
kitaanza rasmi ifikapo Desemba 9, mwaka huu.
Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akiweka jiwe la
msingi katika kiwanda hicho kilichopo Kibaha, Pwani ambapo alisema ugonjwa wa
malaria ni tishio nchini na duniani kote.
Alisema serikali imekuwa ikifanya jitihada
kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Kikwete alisema kiwanda hicho kilianza kutoa dawa
katika kata 72 za Jiji la Dar es Salaam, hivyo kitasaidia kunusuru maisha ya
watu.
Alisema, wazo la ujenzi wa kiwanda hicho alilipata
mwaka 2009 alipokwenda Cuba, baada ya kuiona teknolojia hiyo ya kuua vijidudu
vya malaria na kuifurahia.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC), Dk. Chrisant Mzindakaya, alisema ujenzi wa kiwanda hicho hadi
kukamilika utagharimu dola za Marekani mil. 22.3 na sh bil. 5 zilizotolewa na
serikali.
Alisema kiwanda hicho kiko nyuma ya mpango wa utekelezaji
wa mradi kwa miezi 14, kazi inayoendelea sasa ni ufungaji wa mitambo na
maandalizi ya kupeleka wataalamu wa Kitanzania kwenye mafunzo kwa ajili ya
uzalishaji.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment