Home » » SHULE YA MAKURUNGE YA KILUVYA PWANI YAPUUZA AGIZO LA MH. MULUGO

SHULE YA MAKURUNGE YA KILUVYA PWANI YAPUUZA AGIZO LA MH. MULUGO


Philipo-MulugoAGIZO la Naibu  Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo la kuwataka walimu wote wa shule za serikali la kutowarudisha watoto nyumbani kwa madai ya ada limeonekana kupuuzwa na uongozi wa shule ya sekondari ya Makurunge iliyoko Kiluvya mkoani Pwani.
 Mmoja wa wazazi, James Charles, alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na …… kwa njia ya simu, ambako alisema ni jambo la lusikitisha la kutolewa nje watoto hao wakati wa mtihani na kuwarudisha nyumbani kwa kosa ambalo si la kwao.
 Alisema hiyo ni kawaida ya walimu wa shule hiyo kuwarudisha nyumbani wanafunzi hao japo wizara ya elimu ilikwishatoa tamko kuwa ni marufuku kwa walimu kuwarudisha nyumbani kwa madai ya ada.
 Charles alisema tabia hiyo imekuwa ikiwarudisha nyuma wanafunzi hao kitaaluma kwa kuwa baadhi yao hukaa nyumbani muda mrefu nyumbani wakisubiri wazazi wakitafuta hiyo ada.
 “Hakuna mzazi asiyetaka kulipa ada pia hakuna ugomvi vilevile kufanya hivyo ni kumuadhibu mwanafunzi ambaye hahusiki katika ulipaji wa ada hiyo, mhusika mkuu ni sisi wazazi”alisema Charles.
 Aidha, shule hiyo idaiwa kuwa na udhaifu wa uongozi kutokana na maamuzi mengi ya shule hiyo kufanywa na mwalimu aliyetajwa kwa jina moja la Mende wakati si Mkuu wa Shule hiyo.
 Alipotafutwa Mkuu wa Shule hiyo, Shishila Msengi, ili kutoa ufafanuzi, Mkuu huyo alionekana kutoa kauli zilizokuwa zinakinzana.
 Alisema hajawarudisha nyumbani, mara walirudishwa lakini ni bodi ya shule ndio imefikia uamuzi huo ambako uamuzi huo ulifikishwa kwa Ofisa Mtendaji.
 Ni hivi karibuni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo alisikika akisema ni marufuku kwa walimu kuwarudisha nyumbani wanafunzi kwa madai ya ada, mwalimu atakyebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa