WILAYA ya Kibaha imeanzisha utaratibu wa kutumia mikataba ya kusajili watu
wageni wanaohamia kimakazi katika vijiji na mitaa mbalimbali kwa lengo la
kupunguza na kuondoa kabisa migogoro ya ardhi wilayani humo.
Akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake,mkuu wa wilaya ya Kibaha Halima Kihemba amesema
kumekuwepo na kutokuelewana mara kadhaa kwa baadhi ya wakulima na wafugaji
katika maeneo mengi ya vijijini na uchunguzi ukabaini migogoro hiyo inatokana
pia na watu kuhamia na kujichukulia maeneo bila kufuata taratibu ya matumizi ya
maeneo husika.
Amesema uingiaji huo wa
kiholela unamfanya mtu kujiamulia afanye nini katika eneo analolimiliki hata
kama matumizi ya ardhi hiyo siyo anayotaka kutumia na hivyo kuleta kutokuelewa
kwa upande wa pili mfano anayehamia ni mkulima anaanza kulima wakati wenyeji
wake ni wafugaji.
Kutokana na uingiaji huo
wa kujiamualia Kihemba amesema sasa wilaya hiyo kupitia halmashauri zake mbili
mjini na vijijini wamebuni utaratibu wa kutumia mikataba ambapo mgeni yeyote
akifika atapaswa kujisajili na kuishi kikanuni kama mkataba huo unavyomuelekeza
na endapo atakiuka atawajibishwa moja kwa moja.
Kihemba alitaja moja ya
sharti lililopo kwenye mkataba huo unawataka wageni wote kujisajili kuwa ni
kuheshimu miundombinu yote iliyopo kijijini ama kwenye mtaa na pia atambue
ardhi ni mali ya kijiji au mtaa husika.
Naye Mkurugenzi wa
hamashauri ya Kibaha vijijini Fatuma Selemani amesema hivi karibuni kumekuwepo
na migogoro ya mara kwa mara katika kata za Ruvu,Kwala,Dutumi na hivyo kupitia
mpango huo wa kusaji wageni kimkataba utaweza kupunguza kabisa hali hiyo.
Fatuma aomengeza kuwa
mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji vinne vya Magindu,Gumba,Lukenge
na Mpiji vimeandaliwa kwa mwaka 2010 na kwamba vijiji vingine vitatu vya
Kwala,Mperamumbi na Msua viko kwenye maandalizi ya mwisho mwaka 2012,2013
kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi.
0 comments:
Post a Comment