Home » » MKUTANO MKUU WA TASWA KUFANYIKA DESEMBA 21 NA 22 BAGAMOYO

MKUTANO MKUU WA TASWA KUFANYIKA DESEMBA 21 NA 22 BAGAMOYO







DAR ES SALAAM, Tanzania


MKUTANO
Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) utafanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel,
Bagamoyo mkoani Pwani.


Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wanachama  100, na pia
watakuwepo wadau mbalimbali wa TASWA wakiwemo waandishi wakongwe wa
habari za michezo wambao watapewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano
huo.

Wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili
Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na
masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari za michezo kwa ujumla.

Pia
kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo
ili wawe na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama
ambayo itajadiliwa kwenye mkutano huo.

Kamati ya Utendaji ya
TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa
kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza
iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na
kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe kama ajenda kamili
ya kuanzisha chama hicho kwenye Mkutano Mkuu.

Nia yetu ni kuona
tunapiga hatua za kimaendeleo na kuwafanya wanachama wetu wafurahie
kujiunga na chama hiki na waweze kupata mikopo ya kuwasaidia katika
masuala mbalimbali.

Tunawaomba wanachama wote ambao wanatarajia
kuhudhuria mkutano huo wathibitishe ushiriki wao kwa Katibu Mkuu wa
TASWA kwa njia ya email: mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com. Mwisho
wa kuthibitisha ni Desemba 15, 2012 saa kumi alasiri ili maandalizi
mengine yaendelee na uwepo wao katika mkutano uthaminike.

Wanachama
ambao wanajua hawajalipa ada ni vyema wakafanya hivyo, kwa kuwasiliana
na Mhazini Mkuu wa TASWA, vinginevyo chama kitafanya utaratibu mwingine
wa kuhakikisha ada zao zinapatikana siku ya mkutano.

TASWA
inaendelea na mazungumzo na wadhamini mbalimbali na Jumatatu Desemba 10,
2012 saa tano asubuhi katika mgahawa wa City Sports Lounge Dar es
Salaam itatangaza mdhamini wa mkutano huo.

Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
03/12/2012

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa