Home » » Hatimaye Mkutano wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani uliositishwa hivi karibuni kwa madai ya kugubikwa na mazingira ya rushwa, umefanyika mjini Kibaha.

Hatimaye Mkutano wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani uliositishwa hivi karibuni kwa madai ya kugubikwa na mazingira ya rushwa, umefanyika mjini Kibaha.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdala Bulembo Majura, akisalimia
na mmoja wa makada wa chama hicho Juma Simba, wakati wa sherehe za
kumpongeza kwa ushindi katika uchaguzi w ajumuia hiyo uliofanyika mjini
Dodoma, zilizofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
Kushoto ni Mwenyekiti wa  Jumuiya hiyo Mkoa wa  Dar es Salaam  Angela
Kizigha. Picha na Emmanuel Herman
--
 HATIMAYE Mkutano wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
mkoani Pwani uliositishwa hivi karibuni kwa madai ya kugubikwa na
mazingira ya rushwa, umefanyika jana mjini Kibaha.

Uchaguzi huo
ulishuhudia baadhi ya makada maarufu wa chama hicho wakianguka katika
uchaguzi huo, wakati akiwamo waziri na wabunge walipeta katika nafasi za
uwakilishi katika kamati ya siasa ya mkoa huo.

Uchaguzi huo
uliokuwa ufanyike Oktoba 17, uliahirishwa na hivyo mwenyekiti wa chama
hicho Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao baada ya kuwapo kwa taarifa za
kugubikwa na vitendo vya rushwa.

Siku hiyo Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, 
Mwantumu Mahiza, aliwaeleza wajumbe hao kuwa alipata taarifa kutoka
vyombo vya usalama kuwa uchaguzi huo umegubikwa na rushwa.

Hata
hivyo, juzi uchaguzi huo ulirudiwa kwa ajili ya kuwachagua Katibu wa
Uchumi, Fedha na Mipango, Katibu Mwenezi na wajumbe wa Halmashauri ya
Mkoa, ambapo Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Imani Madega ambaye
aliangukia pua.

Madega alikuwa akiwania nafasi ya Katibu wa
Uchumi, Fedha na Mipango dhidi ya Mbaraka Dau na Haji Abuu Jumaa ambaye
ni Meneja wa Mradi wa Benki ya Kijamii ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM
Taifa, iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete mjini 
Dodoma.

Jumaa ndiye aliyeibuka kidedea katika uchaguzi wa awamu
ya pili baada ya wagombea wote kutopata kura za kutosha kumtangaza
mmojawapo kuwa mshindi. Mlao alisema katika awamu ya kwanza, Madega
akipata kura nane, Dau kura 30 wakati Jumaa aliongoza kwa kupata kura
34.

Katika awamu ya pili, Dau alipata kura 34 na Jumaa kura 37 na
hivyo mjumbe huyo kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Katibu wa
Uchumi, Fedha na Mipango wa CCM mkoani Pwani.

Katika nafasi ya
Katibu Mwenezi,  Mbunge wa zamani wa Kibaha Mjini, Dk Zainab Gama,
aliibuka kidedea katika uchaguzi ambao pia ulirudiwa kwa awamu mbili.

Katika
awamu ya kwanza Dk Gama alipata kura 32 dhidi ya wapinzani wake na kura
walizopata wakiwa ni Mohamed Kiaratu (kura mbili), Philemon Mabuga kura
14 na Jabir Masenga kura 16.

Matokeo hayo ya kura hayakutoa
mshindi na kulazimika kurudiwa ndipo Dk Gama aliweza kuibuka mshindi kwa
kupata kura 43 dhidi ya 28 za Masenga aliyekuwa akitetea nafasi yake.

Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Kisarawe,
Selemani Jafo na Mbunge wa Viti Maalumu, Subira Mgalu waliungana na
makada wengine  kwa kushinda nafasi za ujumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa
wa Pwani.

Mlao aliwatangaza wengine kuwa ni Katherine Katele na
Madega ambaye hata hivyo alikubali nafasi hiyo kwa shingo upande, huku
akidai kwamba hakuwa amepanga kuwania.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa