Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo akisalimiana kwa kumpa mkono mmoja wa wagonjwa mara alipofanya ziara yake ya kushtukiza katika hospitali ya tumbi kwaa ajili ya kuweza kufanya ukaguzi katika mradi wa upanuzi wa hospitali hiyo.PICHA NA VICTOR MASANGU.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
NAIBU
Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo amefanya ziara ya kushtukiza katika
Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na kutoa muda wa wiki moja kwa
mtendaji mkuu wa Shirika la elimu Kibaha kuanza mara moja ujenzi kwa
ajili ya mradi wa upanuzi wa majengo baada ya kubaini umekwama kwa
kipindi cha miaka saba bila ya kuendelezwa kitu chochote hali ambayo
imesababisha kwa sasa eneo hilo kuota nyasi na kugeuka kuwa vichaka.
Jafo
akizungumza kwa masikitiko makubwa na baadhi ya watumishi wa hospitali
ya Tumbi,pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Pwani amechukizwa kuona mradi huo kutelekezwa na kusababisha
miundombinu yake ya majengo kuchakaa kabla hata ya kuanza kutumika
kitendo ambacho amekilaani vikali na kusema suala hilo hawezi kulifumbia
macho hata kidogo.
Jafo
alibainisha kuwa serikali tayari imeshatoa kiasi cha shilingi milioni
600 na fedha hiyo imeshaingizwa katika Ofisi ya Ras Pwani tangu mwaka
jana kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo lakini anashangazwa kuona
mradi huo kusimama, hivyo amewaagiza watendaji wa mamlaka zinazohusika
kukutana na kuliweka sawa jambo hilo kwa lengo la kuweza kuboresha sekta
ya afya.
“Kwa
kweli natoa wiki moja kwa mtendaji mkuu kufanya haraka iwezeknavyo
mradi huu wa upanuzi ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kirefu kukaa
chini na watendaji wenzake wakubaliane na kuweza kuanza mara moja ujenzi
huo maana fedha zipo tu na kwamba tayari tumeshazitoa shilingi milioni
600 sasa sijui nini tatizo kwa hiyo wiki ijayao nataka kuona ujenzi huo
unaanza kuendelea,”alisema Jafo.
0 comments:
Post a Comment