Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa Pwani na watendaji wakuu wa Shirika la Elimu Kibaha ambao Hospitali ya Tumbi ipo chini yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ramani ya upanuzi wa jengo la hospitali ya Tumbi Kibaha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akimsalimiana na mgonjwa ambaye ni mlemavu wa viungo katika Hospitali ya Tumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo mkoani Pwani.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi ameutaka Uongozi wa Shirika la
Elimu Kibaha na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kukaa pamoja na
kufanya Maamuzi ya haraka ndani ya wiki moja wafikie makubaliano ya
uendelezaji wa ujenzi wa jengo jipya la upanuzi wa hospital ya Tumbi
ambayo ni hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani.
Jafo
ameoneshwa kukerwa na ugoigoi wa kufanya maamuzi unaoendelea licha ya
serikali kupeleka fedha kiasi cha sh.milioni 685 katika mwaka wa fedha
2016/2017 lakini mpaka sasa wameshindwa kufanya Maamuzi.
Naibu
Waziri Jafo amesema kitendo hicho kinachelewesha kuwapatia huduma bora
wananchi.Kutokana na hali hiyo, Jafo amewaonya watendaji hao na kuagiza
hadi wiki ijayo wawe wamekamilisha mkataba wa makubaliano na ujenzi
uanze mara moja.
Upanuzi
wa hospitali ya Tumbi unalenga kuimarisha miundombinu ili hospitali
hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi mbalimbali wa mkoa wa pwani
na mikoa mingine hapa nchini kwani kwa muda mrefu hospitali hiyo imekuwa
ikipokea wagonjwa wengi kwa siku ikihusisha pia majeruhi wengi wanao
pata ajali katika barabara ya Morogoro.
0 comments:
Post a Comment