Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Mwamvua Mwinyi,
KATIBU
msaidizi mkuu idara ya organaizesheni ya chama cha mapinduzi (CCM)Makao
Makuu,Steven Kazidi ,ameonya waliokisaliti chama wazi wazi na hadharani
,wakati wa uchaguzi mkuu uliopita na sasa wamejitokeza kugombea nafasi
mbalimbali ndani ya chama majina yao yasipitishwe.
Amesema watu hao walikisaliti chama bila aya wala aibu hivyo hakuna sababu ya kuwapa fursa ya kupitisha majina yao.
Kazidi amesema vikao husika vinavyopitisha majina ya wagombea visijaribu kuwabeba hata kidogo,wanachama na viongozi waliojulikana kukisaliti chama.
Akikumbushia marekebisho ya kanuni na katiba yaliyofanyika hivi karibuni,kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoani Pwani,Kazidi alifafanua kuwa watu walikuwa hadharani sasa wanagombea wasirudishwe.
Kazidi amesema vikao husika vinavyopitisha majina ya wagombea visijaribu kuwabeba hata kidogo,wanachama na viongozi waliojulikana kukisaliti chama.
Akikumbushia marekebisho ya kanuni na katiba yaliyofanyika hivi karibuni,kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoani Pwani,Kazidi alifafanua kuwa watu walikuwa hadharani sasa wanagombea wasirudishwe.
“Tafadhali
,chodechonde waliokisaliti chama na kujitokeza kugombea nafasi za chama
na jumuiya kwa sasa wasipewe nafasi,Natoa wito watu hawa wanajulikana
wasipewe nafasi”alisisitiza Kazidi.
Aidha
Kazidi ,alieleza kwamba wanachama waliochukua fomu za kugombea nafasi
mbalimbali za chama waachane na habari ya safu na kuchafuana kwasasa
wakati hatua nyingine za uchujaji na kupitisha zikiendelea.
Alisema
kila mmoja agombee katika nafasi yake wasipangane safu kwa maslahi ya
watu wanaotarajia kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu 2020 ama uchaguzi
wa serikali ya mtaa 2019 .
Aliwaomba kuacha kujihusisha na rushwa hali itakayosababisha kukatwa majina ya watakaobainika kufanya hivyo.
Katika
kikao hicho hakusita pia kukumbusha marekebisho yaliyofanyika ndani ya
chama ikiwemo kupunguza wingi wa wajumbe wa vikao,mfumo wa kura za
maoni,muundo wa chama ngazi ya mashina na matawi na kata,kutokujwa na
nafasi za kuteua.
Nae
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani anaemaliza muda wake ,Mwinshehe
Mlao,alisema wamemualika katibu huyo msaidizi mkuu idara ya
organaizesheni CCM Makao Makuu ,kwa ajili ya kutoa maelekezo kwa
mabadiliko yaliyofanywa ndani ya katiba ya chama na kanuni za uchaguzi
ambapo anaamini watayafanyia kazi.
Alisema wanachama wote waliogombea wanapewe haki kwani hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake.
Mlao
alisema imefika wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama , kila mmoja
aheshimiwe na haki itendeke ili demokrasia ichukue nafasi yake .
0 comments:
Post a Comment