Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
SERIKALI
imesema kisiwa cha shungimbili kilichopo Wilayani Mafia mkoani Pwani
hakijauzwa kwa kampuni ya Zululand ya Afrika Kusini na badala yake
kimeingizwa katika uwekezaji kupitia kampuni ya Thanda Tanzania Ltd
inayojenga hoteli ya kitalii.
Akijibu
swali la Mbunge wa Mwanakwerekwe (CCM), Ali Said Khamis, leo Bungeni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema
Alisema uwekezaji huo umepitia taratibu zote za Serikali na pindi
utakapokamilika mwekezaji atatekeleza wajibu wake ikiwemo kulipia tozo
zote kwa mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa sheria.
Makani
alisema alisema kisiwa cha shungimbili ni miongoni mwa visiwa 15 ambayo
ni maeneo tengefu yanayosimamiwa na Taasisi ya Hifadhi za Bahari na
Maeneo Tengefu nchini (MPRU).
Mhandisi
Makani alisema MPRU iliianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge na.29 ya
mwaka 1994 ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kusimamia maeneo yote
yaliyotangazwa kuwa hifadhi za Bahari na maeneo tengefu ya bahari.
Aliongeza
kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa ndiyo yenye dhamana ya kuingia mikataba yote ya kimataifa yenye maslahi kwa Taifa.
Aidha
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida,
Martha Mlatta, Makani alisema Serikali inaendelea kuvijengea uwezo vyuo
vya utalii vilivyopo nchini ili kuhakikisha kuwa wahitimu wake wanakuwa
mahiri katika soko la ajira nchini.
“Mfanyabiashara
akitafuta mwajiriwa ni lazima ahakikishe kuwa anaye mwajiri anakuwa na
sifa zote za kumletea faida, hivyo na sisi pia tunataka wahitimu wetu
katika vyuo vya utalii wanakuwa wanapata umahiri wa kutosha ili waweze
kuajiriwa katika nafasi za juu kabisa katika kampuni yoyote” alisema Makani.
Mbunge
Mlatta alitaka swali lake la nyongeza alitaka kufahamu Serikali ina
mikakati ipi katika kuhakikisha kuwa wahitimu wa Tanzania wanapewa
nafasi za juu za kazi katika hoteli za kimataifa

0 comments:
Post a Comment