Na Lilian Lundo –Maelezo.
10/06/2016
Halmashauri ya Mji wa Kibaha imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mji huo kwa sasa ni asilimia 56 kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
Akiongea
kwa njia ya simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Bw. Innocent
Byarugaba amesema kuwa Halmashauri ina jumla ya miradi 11 ya maji ambayo
mitano imekamilika na sita iliyobaki iko katika hatua za mwisho.
“Maji
safi na salama yanapatikana kwa asilimia 56 ikiwa ni juhudi za
Halmashauri za kukabiliana na tatizo la maji na mpaka sasa miradi mitano
imekamilika ambayo hutoa huduma ya maji kwa wananchi,” alisema Bw.
Byarugaba.
Katika
kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji unakuwa bora zaidi, Byarugaba
amesema kuwa jitihada za kukamilisha upatikanaji wa maji unafikia
asilimia 100 ambapo wanaendelea kukamilisha miradi mbalimbali
inayofanywa na Halmashauri hiyo.
Aliongeza
kwa kutaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na Mradi wa maji Mtaa wa
kwa mfipa Galagaza kata ya Msangani, Vikawe kata ya Pangani, Sagale
kata ya Viziwaziwa, Zojosa kata ya Misugusugu na Mwanalugali kata ya
Tumbi.
Aidha
alianisha miradi mingine ya maji inayotegemewa kukamilika kwa mwaka wa
fedha 2016/17 kuwa ni mtaa wa Sofu kata ya Sofu, Muheza kata ya
Mailimoja, Kibenge kata ya Msangani, Kibugalo kata ya Visiga, Kalabaka
kata ya Misugusugu na Mikongeni kata ya Viziwaziwa.
Bw.
Byarugaba alitoa wito kwa kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaokata
mabomba ya maji na kujiunganishia maji kinyemela kwani kwa kufanya hivyo
kunapunguza kasi ya maji na kusababisha watu wengine kukosa maji.

0 comments:
Post a Comment