Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Shirika
la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limefanikiwa
kuunganishia huduma ya maji jumla ya wateja wapatao 183,500 wakiwemo
wateja wapya 3500.
Shirika
hilo bado linaendelea kupokea maombi mapya ya kuunganishia maji wateja
wapya ili kutatua kero inayowasumbua wakazi wa jiji la Dar es salaam na
miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa DAWASCO, Evalistine Lyaro alipozungumza na MAELEZO ili
kupata ufafanuzi wa namna shirika hilo lilivyojipanga katika
kuwaunganishia maji wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo
Mkoani Pwani.
“Shirika
limepunguza viwango vya maunganisho mapya ambapo kwa sasa mwananchi
atalipia kiasi cha Sh. 200,000 na kupata huduma ya maji kwa muda mfupi
na kwa wale ambao wapo zaidi ya umbali wa mita 50 watachangia gharama
kidogo ya vifaa ili waweze kuunganishiwa maji” Evalistine.
Wananchi
wote wa maeneo hayo wanatakiwa kuomba kupatiwa huduma hiyo kwenye ofisi
yoyote ya DAWASCO iliyo karibu nao au wasiliana na kituo cha huduma kwa
wateja kwa kupiga simu namba 022-2194800 au 0800110064 ambapo huduma
hiyo ni ya bure.
Zoezi
hilo la kuwaunganishia maji wateja wapya linafuatia kutekeleza agizo la
Serikali la kuwafikia wateja Milion Moja katika mwaka huu wa fedha
2015/2016 ambalo limeanza rasmi Januari 01, 2016 na limegawanyika katika
awamu kuu nne.
Awamu
ya kwanza ya kuwaunganishia maji wateja hao itawahusisha wateja wote
walioko katika maeneo ambayo kwa sasa yanapata maji na kuna miundo mbinu
ya mabomba karibu, awamu ya pili itahusu maeneo ambayo yamepitiwa na
mabomba makubwa ya maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa
sababu ya kukosekana kwa miundo mbinu ya usambazaji.
Wakati
awamu ya tatu itahusisha maeneo yote yaliyopitiwa na mradi maarufu wa
mabomba ya Kichina, Maunganisho katika awamu hii yataanza baada ya
kukamilika kwa Miradi ya Ruvu Chini na Ruvu Juu na awamu ya nne itaanza
katika maeneo yote ambayo kwa sasa hakuna miundo mbinu ya Maji na yako
mbali kutoka katika mabomba makubwa.
Aidha,
wananchi wote wa maeneo hayo wanahamashishwa kuchangamkia fursa hiyo ya
kuunganishiwa maji ili waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na
kuhakikisha wanapata maji safi waweze kupambana na magojwa mbalimbali
ambayo ni adui mojawapo wa taifa.
0 comments:
Post a Comment