Mwanamuziki
nguli wa dansi kutoka DRC Congo, Papaa Wemba kushoto akiimba na
kucheza sambamba na madansa wake jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye
tamasha la muzuki la Karibu Music Festival msimu wa pili linaloendelea
katika viwanja vya Mwanakalenge,mjini Bagamoyo. (Picha zote na Andrew
Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA]
Mwanamuziki kutoka Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa, Papaa
Wemba, ameweza kuonyesha ukomavu wake kwenye muziki wa dansi licha ya
kuwa na uri wa miaka 66, kwa kupiga shoo ya aina yake usiku wa kuamkia
leo kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015 linaloendelea ndani ya
viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo-Tanzania.
Katika
shoo hiyo, Papaa Wemba aliweza kupanda jukwaani akiwa na bendi yake na
kupiga nyimbo zaidi ya tano zilizokonga nyoyo mashabiki lukuki
waliofurika ndani ya viwanja hivyo vya Mwanakalenge mjini hapa.
Papaa
Wemba ambaye anatamba kwa muda mrefu na wimbo wa “Show Me The Way”
ameweza kuwa miongoni mwa wasanii wa muziki wa dansi kutoka DRC Congo
kufika Tanzania kwa mara ya pili sasa kwa vipindi tofauti huku
watanzania wengi wakionyesha kumkubali na kufuatilia muziki wake mara
kwa mara.
Baada
ya shoo hiyo Papaa Wemba aliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa
wingi na kumuunga mkono katika muziki wake ambapo alieleza kuwa tamasha
hilo la Karibu Music Festival licha ya kuwa change kwa kufanyika mwaka
wa pili, huko linakoelekea litakuwa kubwa zaidi na kuwa maarufu.
Katika
shoo hiyo, Papaa Wemba aliimba nyimbo zaidi ya nne huku akiimba pia
vibao kadhaa vilivyowahi kutamba miaka ya nyuma pamoja na nyimbo
mbalimbali zikiwemo mpya.
Tamasha
hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati,
linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na
Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana
na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja
na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication,
Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
Papaa
Wemba akiimba jukwaani kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015,
usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
Papaa
Wemba akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) kwenye tamasha la
Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya
Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
Wanenguaji wa Papaa Wemba wakishambulia jukwaa kwa style ya aina yake ambao walikuwa kivutio katika tamasha hilo..
Sebene likiendelea jukwaani..
Host
wa tamasha la Karibu Music Festival 2015, Mc Lulu akipata kuimbisha
mashabiki waliofurika katika tamasha hilo kwa kuimba sambamba na Papaa
Wemba (Hayupo pichani) kibao cha "Show Me the way"..
Papaa Wemba katika ubora wake..
Dansa akifanya yake jukwaani..
Papaa Wemba..
Mwenyekiti
wa tamasha la Karibu Music Festival, Amarido Charles (kushoto) akiwa
pamoja na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Bodenim 'Bo' katika viunga
vya tamasha hilo viwanja vya Mwanakalenge..
0 comments:
Post a Comment