Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Msanii nyota wa Afrika Kusini, Bo Denim "Bo" akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la msimu wa pili la Karibu Music Festival..!
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA]
Mwanamuziki nyota kutoka Afrika Kusini Bo Denim maarufu ‘Bo’
amewashukuru waandaji wa tamasha la Music Festival linalofanyika kila
mwaka mjini hapa huku likihusisha vikundi na wanamuziki mbalimbali
kutoka mataifaa tofauti ya Afrika nan je ya Afrikaa.
Bo
ambaye usiku wa jana Novemba 7, aliweza kupiga shoo hiyo kwa kiwango
cha Kimataifa, alipata shangwe kwa mashabiki waliofurika kushuhudia
tamasha hilo mjini hapa.
Baada
ya shoo hiyo Modewji ilipata kufanya naye mahojiano ambapo amepongeza
muziki wa Tanzania wakiwemo wasanii wanaovuma nje ya mipaka ya
Tanzania. “Wasanii wa Tanzania wanauwezo mkubwa. Nimeshuhudia kundi la
Weusi wamefanya vizuri sana” ameeleza Bo.
Tamasha
hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati,
linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na
Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana
na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja
na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication,
Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
Bo akipagawisha mashabiki ...
Mambo yalikuwa hivi ..
Host wa Karibu Music Festival 2015, Jazzphaa Nassor na Lulu wakishoo love wakati wa shoo hiyo ya "Bo"..
0 comments:
Post a Comment