Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi
ya waombelezaji katika msiba huo. Kulia ni Ridhiwani Kikwete mgombea
Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo Majid Mwanga, mkuu wa wilaya ya Nachingwea Pololet Mgema na
mgombea ubunge Jimbo hilo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Matayo Torongei wakiwa kwenye msiba huo.
Na John Gagarini, Lugoba
Wagombea wa nafasi za uongozi hapa
nchini wametakiwa kukubali matokeo mara uchaguzi utakapofanyika Oktoba
25 mwaka huu kwani kuna maisha mengine baada ya uchaguzi, na kuendelea
kufanya kampeni zao huku wakiendelea kuhubiri na kulinda amani iliyopo
kwani wana nafasi kubwa ya kuwashawishi wafuasi wao wasifanye vurugu au
kufanya vitendo vinavyosababisha uvunjifu wa amani.
Pia wagombea watakaoshindwa kwenye
uchaguzi mkuu wameombwa wakubali matokeo kwani kwenye washindani lazima
kuwe na washindwa ili kuondoa hali ya mafarakano kwani kwa wale
watakaoshindwa wasipokubali matokeo wanaweza kuleta uvunjifu wa amani.
Hayo yalisemwa katika Kijiji cha Maviayangombe kata ya Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani na Askofu mkuu wa Dayosisi ya Morogoro ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jacob Mameo Ole Paulo wa Dayosisi ya Morogoro wakati wa mazishi ya mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa wafugaji Laban Moreto, Karokya Moreto (33) ambaye alikuwa mwanajeshi wa kikosi cha 04/691 cha Mtwara.
Pwani na Askofu mkuu wa Dayosisi ya Morogoro ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jacob Mameo Ole Paulo wa Dayosisi ya Morogoro wakati wa mazishi ya mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa wafugaji Laban Moreto, Karokya Moreto (33) ambaye alikuwa mwanajeshi wa kikosi cha 04/691 cha Mtwara.
Askofu Ole Paulo alisema kuwa
wagombea hao wanauwezo wa kudumisha amani kwa kuhubiri au kuingiza nchi
kwenye machafuko endapo watayatumia vibaya majukwaa wakati wa kipindi
hichi cha kampeni za uchaguzi.
“Wanapaswa kuhubiri amani na kuacha
kutumia maneno yatakayo haribu amani ya nchi iliyopo ambayo imedumu kwa
kipindi kirefu tangu nchi ilipopata uhuru miaka zaidi ya 50 hivyo
itakuwa ajabu ivunjwe kisa kuwania uongozi tu,” alisema Askofu Ole
Paulo.
Alisisitiza kuwa vyama vya siasa
vinapaswa kupingana kwa hoja na kwa malumbano ambayo hayana maana bali
yanaweza kuleta mitafaruku isiyokuwa ya lazima hasa kwa wale
wanaoshindwa kwani wanapaswa kukubali matokeo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa amesikitishwa na kifo cha
marehemu ambaye alikuwa ni ndugu kwani wamekuwa wakiishi kama familia
moja na walikuwa na ushirikiano mkubwa baina ya familia zao.
Ridhiwani alisema kuwa kifo hicho
ni pigo kwa familia hiyo pia kwa Taifa kwani alikuwa ni mtumishi wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na alikuwa mtaalamu wa rada hivyo
pengo lake haliwezi kuzibika kikubwa ni kumwombea marehemu.
Rais Dk Jakaya Kikwete alituma
salamu za pole kwa familia hiyo kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete na kusema kuwa anatoa pole na Mungu awape nguvu katika
kipindi hichi kigumu cha maombolezo na yuko pamoja nao.
Alisema kuwa Rais alishindwa
kuhudhuria msiba huo kwani kwa sasa yuko nje ya nchi lakini pindi
atakaporudi ataitembelea familia hiyo kwa ajili ya kuifariji kufuatia
kifo cha mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa kabila wafugaji
Naye mgombea Ubunge Jimbo la
Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mathayo
Torongei alisema ili amani iendelee kuwepo ni vema dola ikatenda haki
badala ya kupendelea upande mmoja.
Marehemu alifariki kwa ajali baada
ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi la mbele na kusababisha
ajali iliyopelekea kifo chake siku ya Septemba 16 mwaka huu huko Mtwara.
Ameacha mke na watoto watatu.
Baadhi ya Wazee wakiwa wamekaa kwenye msiba huo huko kijiji cha Maviyangombe Lugoba wilayani Bagamoyo.
0 comments:
Post a Comment