Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea huyo akiwapungia wananchi wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni hizo.
|
VICTOR MASANGU, KIBAHA VIKUNDI
KATIKA kuunga juhudi za serikali kupambana na kupunguza janga la umasikini linalowakabili vijana
na wakinama Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya
chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala
hilo endapo akichaguliwa awamu ya pili ambapo atatenga shilingi milioni
700 katika jimbo lake kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya ujasiriamali.
Mgombea huyo ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni katika jimbo la Kibaha mjini ambapo amesema lengo lake kubwa ni kuvisaidia mtaji vikundi vyote vya ujasiriamali lengo ikiwa ni kuhakikisha anasaidia vikundi hivyo kuanzia ngazi zote za vijiji hadi jimbo.
Koka
alisema kwamba anatambua katika jimbno lake la kibaha mjini kuna
vikundi vingi vya ujasiriamali hivyo atahakikisha kwamba anaviwezesha
katika kuvipatia mtaji kwa ajili ya kuweza kukuza uchumi wananchi wa
Kibaha pamoja na Taifa kwa ujumla.
“Kwa
upande wangu mimi endapo wakinipa nafasi ya kuongoza tena katika jimbo
la kibaha mjini nitahakikisha kuwa ninashirikiana nao kw ahali na mali
ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kuanzia ngazi zote za kaya hadi ngazi ya Taifa kwa hiyo hiyo ndio moja ya mikakati yangu.
Pia
alisema kwamba katika kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuachana na
tabia ya kuwa tegemezi ataweka mipango mikakati ya kuongeza viwanda
vingi amabvyo vitaweza kutoa fursa ya ajira kwa vijana sambamba na
kuongeza wigo mkubwa ya kuleta maendeleo kupitia sekta mbali mbali.
Aidha
Koka alisema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa ya uhaba wa
maji ameshaanza juhudi za makusudi za kuweza kushirikiana na serikali
kutandaza mabomba ili waannchi wa kibaha mjini pamoja na amneo mengine
ya jirani waweze kuondokana na kero hiyo ya maji.
Aidha
mgombea huyo amebainisha katika suala la kukuza uchumi atahakikisha
analivalia njuga suala la miundombinu ya barabara ili kuweza kurahisiha
shughuli mbali mbali za biashara kwa wananchi wake wa jimbo la Kibaha
mjini pamoja na kuweka mikakati kaabambe kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ya kuongeza idadi ya zahanati na vituo vya afaya ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.
Mpaka sasa Mbunge huyo wa jimbo la Kibaha mjini katika
kipindi chake cha miaka mitano iliyopita ameshavisaidia vikundi mbali
mbali vya ujasiriamali zaidi ya 175 ambavyo ameshatumia gharama ya kiasi
cha shilingi milioni 230.
0 comments:
Post a Comment