Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea
wa jimbo la kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Sylivesta
Koka akisalimiana na wananchi wa kata ya msangani kabla ya kuanza kwa
mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi.
Wananchi wakiwa wanashangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.(Picha zote na Victor Masangu)
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Kibaha Maulid Bundala akiwaonyesha wananchi
waliohudhulia katika mkutano huo moja ya kadi ya chadema iliyorudishwa
na mwanachama wa chadema, kulia kwake ni mgombea ubunge jimbo la Kibaha
mjini Silvestry Koka.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MGOMBEA
ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestery Koka amesema kwamba endapo
akichaguliwa na wananchi atahakikisha analivalia njuga suala la
changamoto inayowakabili wakinamama wajawato kwa kujenga wodi za
kujifunguliwa pamoja na kuongeza vifaa tiba sambamba na kupatiwa
matibabu bure ili kupunguza ongezeko la vifo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwa wananachi wa kata ya Msangani
mgombea huyo amesema kwamba wakinamama wajawazito wamekuwa wakipata
usumbufu mkubwa wakati wa kujifungua na wakati mwingine wanapoteza
maisha hivyo ataweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma ya afya
lengo ikiwa ni kuokoa maisha yao.
Koka
amebainisha kwamba mpango huo upo katika ilani ya chama cha mapinduzi na
utekelezaji wake tayari umeshaanza kufanyika sambamba na kuongeza kasi
ya ujenzi wa zahanati ili kuweza kuwasogezea huduma kwa urahisi wananchi
wasipate shida ya kupatiwa matibabu.
Aidha
alisema kwamba katika kuboresha sekta ya afya ataweka utaratibu mzuri wa
kuhakikisha wazee wote wanapatiwa matibabu bure bila ya kupaata
usumbufu wowote na kuwa atakuwa anafanya ziara za mara kwa mara
kutembelea zahanati vituo vya afya pamoja na hospititali ili kuweza
kubaini changamoto.
Akizungumzia
kuhusiana na changamoto ya maji katika kata ya Msangani mgombea pamoja
na mikakati yake aliyojiwekea kuondokana na kero hiyo mgombea huyo
alisema kwa sasa kuna miradi ya maji
ipatayo 14 ambayo imeshatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano
iliyopita na lengo la kuweza kutatua changamoto ya maji.
Kwa
upande wao wananchi wa kata hiyo ya Msangani akiwemo Said Mohamed
na Rashid Abed awakusita kuzungumzia changamoto zinazowakabili
hususan suala la maji ambalo kwa upande wao limekuwa ni kero kubwa
kutokana na kutembea umbali wa kilometa nane kwa ajili ya kwenda
kufuata maji.
Walisema
kwamba kwa sasa wana imani endapo mradi huo wa maji ukikamilika utaweza
kuwanufaisha kwa kisi kikubwa na kutatua kero ya maji ambayo imekuwa ni
kilio cha siku nyingi kwa wakazi wa kata ya msangani.
“Kwa
upande wetu kwa sasa tunaona juhudi ambazo zinafanywa na mbunge ambaye
alimaliza muda wake tumeshuhudia baadhi ya maeneo wameshaaza kupata maji
safi na salma hivyo kitu kikubwa kwa mgombea ambaye tutamchagua
alitilie mkazo suala la maji ili tusiweze kusumbuka kutembea umbali
mrefu,”alisema wananchi hao.
Wananchi
wa kata ya Msangani kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali
mbali katika sekta ya afya hususan wakinamama wajawazito pamoja na
huduma ya maji hivyo kunahitajika kufanyike juhudi za makusudi kwa
viongozi watakaochaguliwa kuhakikisha wanatafuta njia mbadala
kuzitatua kero hizo.
0 comments:
Post a Comment