Home » » WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WATOA KIJASHO NI BAADA YA KUPEWA ZOEZI LA KUTAFUTA VITU VILIVYO FICHWA NA MWISHO KUPANDA MITI .. CHEKI HAPA

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WATOA KIJASHO NI BAADA YA KUPEWA ZOEZI LA KUTAFUTA VITU VILIVYO FICHWA NA MWISHO KUPANDA MITI .. CHEKI HAPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Ni Siku ya Nane ambapo Shindano la Shujaa wa Chakula linazidi kupamba moto zaidi ambapo hapa washiriki wanapata kazi ambayo ni changamoto kubwa kwao.. zoezi hilo ambalo liliitwa KOMBOLELA liliwataka Mama Shujaa wa Chakula kutafuta vitu vilivyofichwa Sehemu nne na mwisho kupanda miti katika sehemu ya tano ambayo nayoo ilikuwa imefichwa.. 
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alishuhudia zoezi hilo .. ambapo kazi walizo fanya Mama Shujaa ni pamoja na Kumwagilia tofali na kuchukua Jembe,Kusafisha duka na kuchukua Mbolea,Kuchukua Miche, kulima na kuchukua maji na Kupanda miti..
Sasa ilikuwa kuwajee.... jiunge hapa..
 Pamekucha sasa hapa ambapo washiriki wa Shindano la  Mama shujaa wa chakula, Linalo endeshwa na Shirika la Oxfam kupitia Programu ya Grow na kipindi kinachoruka katika Runinga Chanel ya ITV kuanzia Saa 12:30 Jioni na kurudiwa Saa 11:30 Asubuhi hapa wakipewa muongozo wakazi na zoezi
Mkurugenzi Mkazi wa wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitazama zoezi la Kombolela kijijini Kisanga
Hapa Mama shujaa wanaoneshwa Ramani ambayo ndipo watavikuta vitu hivyo
Hapa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula wakisoma maelezo ya hatua ya kwanza
Kwa uhakika mkubwa washiriki wa Shindano la mama Shujaa wa Chakula wakidhani kuwa nyumba waliyo ambiwa wanatakiwa kuwa ndiyo hiyo kumbe walikuwa wamechemka na baadae walifukuzwa na wananchi ambao ndio wakazi wa eneo hilo.
Hili ni kundi la kwanza ambalo walikuwa na kazi ya kumwagilia maji matofali
Kundi hili wao ndio kwanza wanasoma maelekezo ya nini wanataka kufanya
Hii ni sehemu ya Nne ambapo kundi hili lilikuwa na kazi ya kulima na kisha kuchukua maji
Kombolela ndio hiyoo imeanza na washiriki wote sasa wanakimbia kutafuta sehemu ya kwanza
Hii ni Sehemu ya tatu ambapo washiriki wa Mama shujaa wa Chakula wakiwa wapo sehemu ya duka ambapo walitakiwa kufanya kazi ya kusafisha mazingira na kupewa mbolea ... cha kushangaza sasa hapa hakuna kundi hata moja lililokumbuka suala la Mbolea.
Hili kundi lililokuwa la kwanza kufika katika eneo la miche
Hapa sasa kama anafukuzwa mwizi... Hapa Kombolela limeshika sehemu yake hapa wanakimbilia sehemu ya tatu kwenye miche
Kundi hili ndilo lililofanikiwa kufika katika sehemu ya mwisho ambayo ilikuwa ni ya Tano ... lakini....
Hapa wanamoyo kungoja kuambiwa wameshinda na waendelee na jambo jengine lakini.. wakaambiwa kuna kitu wamesahau hapa ambacho ni Mbolea .. iliwalazimu warudi tena dukani kuchukua mbolea ili waendelee kupanda miti
Kundi la pili sasa hao wanapanda miti
Kundi la kwanza nao wanapanda miti
Kundi la nne nao wanapanda miti sasa
Kundi la Tano na la mwisho nao wanapanda mti katika Ofisi mpya ya Serikali ya Kijiji cha Kisanga
Kushoto ni Mtendaji na Mwenyekiti wa Kisanga wakiangalia washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula wakipanda mti

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa