Home » » HOT! WASHIRIKI WA SHIMNDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAJIANDAA NA FASHION SHOW NA KUBURUDIKA NA NGOMA KIJIJINI KISANGA .. CHEKI HAPA

HOT! WASHIRIKI WA SHIMNDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAJIANDAA NA FASHION SHOW NA KUBURUDIKA NA NGOMA KIJIJINI KISANGA .. CHEKI HAPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Ni Siku ya 9 ambapo Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaendelea ... utashangaa sana kuwa umezoea kuona kuwa akina mama hawa wanafanya shughuli za Kilimo lakini leo , akina mama hawa wanajiandaa na Fashion Show kubwa kabisa ambapo wanakijiji cha Kisanga na wakazi wa Jirani watapata show hii kabambe kabisa .. Lakini hapa leo wanajiandaa kwa ajili ya Fashion Show.. 
Sasa katika Fashion Show hii wakina mama shujaa wanaenda kuonesha maonesho ya Mavazi, Mafunzo ya Unyago na Muziki wa Asili wa Kizaramo... Kipindi hiki  Muhimu kabisa ambacho kimeandaliwa na Oxfam kupitia katika Programu yao ya Grow na kauli mbiu ni kwamba Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo Inalipa, na Kuruka katika Chanel ya ITV  kuanzia saa Kumi na mbili na nusu Jioni na Kurudiwa Saa tano na nusu asubuhi ...hivi ndivyo ilivyokuwa .....
 Washiriki wa Shindano la mama Shujaa wa chakula wakiwa wanasukana na kufumuana nywele ikiwa ni maandalizi ya Fashion Show
 Maandalizi yanaendelea huku wasusi na walembaji maalum wakiwa wanawaandaa mama shujaa wa chakula
 Upendo Mhomisoli mshiriki kutoka Njombe akilia kwa kile alichodai kuwa washiriki wenzake wanamdai ... baadae alinyamaza mwenyewe na kuendelea kulembwa
 Wamependezaa.. washiriki wakiwa katika picha ya pamoja
 Huu ulikuwa ni muda ambao washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa 4 2015 wakiwa wanajifunza mila na Desturi za Wazaramo hapa walielezwa juu ya unyago kwa wasichana
 Hapa kwa Mikogo wakifanya mazoezi ya kutembea katika onesho la Mavazi
 Wenyeji wa Kisanga wakiwaeleza washiriki wa shindano la  Mama shujaa wa Chakula juu ya Unyago
 Burudani ya Ngoma inaendelea
 Ni full Sapraiz na kuselebuka
 Mwali anatolewa sasa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa