Home » » MECHI KALI YA MPIRA WA MIGUU VUTA NIKUVUTE KATI YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA NA WANAKIJIJI CHA KISANGA YAWAVUTA WENGI .. HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA

MECHI KALI YA MPIRA WA MIGUU VUTA NIKUVUTE KATI YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA NA WANAKIJIJI CHA KISANGA YAWAVUTA WENGI .. HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mambo yanazidi kunoga katika Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne Shindano linalo endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake Inalipa. 
Katika tukio la leo na la kusisimua washiriki wa shindano la Mama shujaa wa chakula walicheza mpira wa Miguu na wenyeji wao wa Kijiji cha Kisanga ambapo Mechi ilikuwa ni ya Vuta ni kuvute , lakini wanakijiji hao waliibuka washindi kwa Goli moja kwa Nunge Dhidi ya Mama Shujaa hao..
Kipindi hiki cha aina yake na chenye kuvuta wengi kinaruka pia katika Runinga yako chanel ya ITV kuanzia Saa 12:30 Jioni na Marudio saa Tano asubuhi hutakiwi kukosa 
Na hivi ndivyo ilivyokuwa... 

 Hii ni zaidi ya Burudani Mama Shujaa wa Chakula pamoja na Mwanakijiji wanachuana vikali hapa .. hii ni zaidi ya utamu
 Kikosi Cha Mama Shujaa wa Chakula wakiwa katika Picha ya pamoja kabla ya Mechi kuanza
Hiki ni Kikosi Cha wanakijiji wa Kijiji cha Kisanga wakiwa katika picha ya Pamoja  kabla ya Mpira kuanza
 Wakipasha kabla mechi haijaanza
 Mpira Ukikaribia kuanza
 Tunaanzia wapi
 Mchaka mchaka umeanza hapa ni full kukimbizana kama swala .. wanakijiji wanakomaa na akina mama shujaa wakiwa wamekomaa ni pata shika
 Hatareeee.... hapa mama Shujaa wa Chakula anapigaaa mpira hapa wanakijiji wanajiandaa kuchukua mpira ni kiki la hataree kabisa

 Pembeni Mashabiki kibao mpira unaendelea kwa kasii ya ajabu
 Mama Shujaa wanapata maji kwanza kwa sababu daah... hiii si ya mchezo
 Goooooooooooooooo......................dah Mama shujaa wanalizwa hapa kwa kupigwa bao moja na wanakijiji ... wachezaji wa Timu ya Kijiji cha Kisanga wanafurahia hapa
 Mashabiki haoo ... Hii ni zaidi ya mechii

Usikose kipindi kijacho....

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa