Home » » HOT! WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAFANYA MAIGIZO JUU YA ARDHI PEMBEJEO NA MASOKO , UNGANA NASI HAPA..

HOT! WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAFANYA MAIGIZO JUU YA ARDHI PEMBEJEO NA MASOKO , UNGANA NASI HAPA..

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Usikose kabisa kutazama kipindi cha Mama shujaa wa Chakula kinachoruka kupitia Ruinga yako Chanel ya ITV kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015  Kila siku saa kumi na mbili Jioni na Marudio Saa Tano na nusu asubuhi... hii si ya kukosa...
Kumekucha ambapo washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa chakula 2015 Shindano linaloletwa kwenu na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni ile ile Wekeza kwa wakulima wanawake wadogo wadogo inalipa wakiwa pamoja na waandaaji wakipindi na watangazaji ambapo mama shujaa wa chakula walipewa zoezi dogo la kuchagua kitu gani wataongelea kati ya mada zinazohusu Masoko, Ardhi au Pembejeo.
 Tunatambua kuwa katika ardhi wanaume ndio wanakuwa juu katika maamuzi katika kipengele hiki inaonesha kuwa washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula  kundi namba tatu wanaigiza juu ya ardhi ambapo Mume anauza Shamba na kutumia pesa hizo Bila hata ya Kumshirikisha Mke wake..
 Kilimo ni Uti wa Mgongo na Tukiwawezesha wanawake katika kilimo kwa hakika tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa, Hapa kundi namba tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakiigiza juu ya Pembejeo na Elimu juu ya Kilimo Bora.
 Mambo yanapamba moto sasa Katika kijiji hiki cha Kasanga ambapo Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wanatoa Elimu kupitia Maigizo, Hili ni Kundi namba mbili ambao wao kupitia Igizo lao wanaonesha Masoko ni Jinsi gani mnunuzi wa zao la Mihogo anataka kuwalalia bei wakulima ambapo kwa pamoja wakulima wamekomaa na wanasisitiza kuuza Mihogo kwa bei wanayotaka wao.
 Hapa ilikuwa ni kujikumbusha ni Jinsi Gani wataigiza katika swala zima la Masoko , Hili ni kundi namba mbili la washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula linaloletwa kwenu na Oxfam kupitia Kampeni yake ya Grow na kurushwa Moja kwa Moja katika Runinga ya ITV kuanzia saa Kumi na mbili Jioni  na Marudio na Kurudiwa Asubuhi saa tano na nusu ITV.
 Hili ni Kundi namba Mbili ambao wao wanaigiza juu ya Haki za Ardhi hapa wakifanya Mazoezi ya kuigiza juu ya mada ya Haki ya Ardhi.
 Hiki ni Kikundi namba tatu hapa wakijadili Jinsi ya kuigiza igizo la Pembejeo..

Kumbuka Kipindi hiki Kinaruka katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV Kuanzia saa Kumi na Mbili jioni na Marudio saa Tano na nusu asubuhi...

Imeletwa kwenu na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow..
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa