Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na
Benedict Liwenga-MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amefurahishwa na uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi
vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria kilichopo eneo la viwanda, Tamco-Kibaha
mkoani Pwani ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali iliyojipangia ya kupambana
na kupunguza vifo visababishwavyo na ugonjwa huo.
Uzinduzi
huo ulifanywa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Nchi zinazopambana na Malaria (ALMA).
Katika
uzinduzi huo, Rais Kikwete ameishukuru nchi ya Cuba kwani wao ndiyo walikubali
kutoa wataalamu pamoja na teknolojia ili kuisaidia Tanzania kuendeleza sekta ya
madawa ikiwemo kupambana dhidi ya ugonjwa wa malaria pamoja na kuwafundisha
wataalamu wa Tanzania ili waweze kuendeleza kiwanda hicho.
Rais
Kikwete alieleza kwamba, akiwa nchini Cuba mnamo Novemba 2009 alitembelea
viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali za kibaiolojia kikiwemo kiwanda cha
Biolarvicides cha LABIOFAM SA kinachomilikiwa na Serikali ya Cuba hivyo
Serikali hiyo ilipokubali awamu ya kwanza ilipanga kujenga kiwanda cha
Biolarvicides kwa lengo la kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza malaria ambapo
mradi huo ndo umezinduliwa rasmi tarehe 2 Julai mwaka huu na pia katika awamu
ya pili ilikuwa ni ujenzi wa viwanda vya kuzalisha dawa mbalimbali kwa ajili ya
kutibu na kuzuia magonjwa ya binadamu na wanyama na mwisho ni awamu ya tatu ya
ujenzi wa viwanda vya dawa na vyakula vya ziada yaani Food supplement kwa ajili
ya watu wenye magonjwa ya kudumu na kuzalisha mbolea za kibaiolojia
(bio-fertilizers).
"Chimbuka
la ujenzi wa kiwanda hiki ni ziara yangu niliyoifanya nchini Cuba, ndipo
niliona kuna umuhimu wa kuiomba Serikali ya Cuba itusaidie kutupatia teknolojia
pamoja na wataalamu lakini pia niliagiza Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC)
wajenge ushirikiano kwa ajili ya kutengeneza kiwanda nchini Kwetu na matokeo
yake ndo haya", alisema Dkt. Kikwete
Rais
Kikwete alimshukuru Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Jorge Luis Lopez kwa
ushirikiano mkubwa aliouonyesha kwa kuisaidia Tanzania katika kuhakikisha
kwamba kiwanda hicho kinawepo nchini na kwa ukarimu wao pasipo tamaa ya kutoa
teknolojia hiyo, licha ya nchi yao kutakuwa tajiri wao walitupati teknolojia
hii na walishirikiana nasi katika ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na wataalamu
"Huu
ndiyo urafiki wa kweli na udugu nakuomba Balozi unifikishie salamu zangu za
dhati na shukurani zangu mimi pamoja na watanzania wote kwa ajumla kwa Rais
Raul Castro kwa mchango wake mkubwa kwa nchi yetu Tanzania", Alisema Dkt.
kikwete.
Naye
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Jorge Luis Lopez ameziomba nchini
nyingine ziweze kuiga ushirikiano mkubwa wa Serikali ya Tanzania na Cuba na pia
kwa niaba ya Serikali yake amemshukuru Rais Kikwete kwa utendaji kazi wake
mzuri, uhusiano mzuri ambao ameujenga na kati ya Tanzania na Cuba.
Naye
mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia na Mwenyekiti wa
Umoja wa Nchi zinazopambana na Malaria (ALMA) na ametoa pongezi zake za dhati
na kueleza kwamba, hiyo ni hatua nzuri na kusema kuwa kushuka kwa idadi ya vifo
nchini Tanzania ni ishara ya uongozi mzuri na bora wa Rais Kikwete na ishara
nzuri kwa kuiacha nzuri katika mahali pazuri pamoja mahali pazuri dhidi ya
umaskini
Aidha,
ameeleza kuwa uwepo wa kiwanda hiko itakuwa ni ishara nzuri ya mapambano na
yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa nchi zinazopambana (ALMA) dhidi ya malaria
atazihamasisha nchi nyingine kutumia Afrika waweze kutumia mazao yatokanayo na
kiwanda hicho.
Kampuni
ya Tanzania Biotech Products Limited ni Kampuni iliyoundwa kwa ajili ya
kuendesha Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya mbu wanaoeneza
malaria kilichopo Kibaha, Pwani ambacho kimejengwa kwa kushirikiana na Kampuni
ya LABIOFAM SA ya Cuba a kiwanda hiki kinatokana na agizo l Rais Kikwete
alilolito Januari 4 , 2010 kwa shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) baada ya
ziara yake nchini Cuba.
0 comments:
Post a Comment