Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kibao
kinacho elekeza eneo la mradi wa viwanda wilayani Kisarawe mkoani Pwani
lililopo Visegese. Mradi huo unaendeshwa na Halmshauri hiyo na wabia wa
Kampuni ya World Map
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro
(kushoto), akizungumza na viongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe,
Wabia wa eneo la mradi wa Kampuni ya World Map na wawekezaji kutoka
nchini China waliofika wilayani humo jana kuangalia fursa za kuwekeza
viwanda katika eneo hilo. Kulia ni Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka
TIC, Elibariki Ngorovily.
Wawekezaji
kutoka China wakiwa katika mkutano na uongozi wa wilaya ya Kisarawe na
wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map kabla ya kwenda kuona
eneo la mradi wa viwanda. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa
Makampuni ya Huallan 'Huallan Group', Tu Huobao, Mkurugenzi wa Masoko wa
Kampuni hiyo, Apple Ye, Huang Haitao na Meneja Masoko, Nara Zhou.
Mkurugenzi
wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko (kulia), akizungumza
katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wawekezaji hao. Kutoka kushoto
ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro, Ofisa
Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily, Mkuu wa Wilaya
ya Kisarawe Subira Kigalu, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Adam Ng'imba (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko na Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu akizungumza katika mkutano huo.
Wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map na viongozi wa idara mbalimbali za wilaya hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakuu wa idara wa wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye
mkutano huo.
Mkutano na wawekezaji ukiendelea.
Maofisa wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map wakiwa kwenye mkutano huo.
Miundombinu ya barabara inavyoonekana eneo la mradi.
Katapila likiwa eneo la mradi kutendeneza miundombinu ya barabara.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro
(katikati), akiwaonyesha ramani ya eneo la mradi wawekezaji hao. Kushoto
ni Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
Mazungumzo eneo la mradi.
Sehemu ya eneo la mradi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Subira Kigalu (katikati), akiwa katika picha ya
pamoja na wawekezaji hao na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na wabia wa
mradi huo kutoka Kampuni ya World Map.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
KATIKA
kukuza uchumi kwa wakazi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mkoani
Pwani mradi wa uendelezaji wa viwanja katika mji mdogo wa Kisarawe uliopo Kijiji cha visegese umeanza kupata wawekezaji kutoka nchini China ili kusaidia kuendelea wilaya hiyo kwa kujenga viwanda.
Wilaya hiyo kwa kushirikiana na wabia kutoka kampuni ya world Map wameweza kupima viwanja zaidi ya 250 katika kijiji hicho kwa ajili ya viwanda na
Kutangazwa katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi na kituo cha
uwekezaji Tanzania (TIC), na hatimaye kuanza kupata wawekezaji ambao
wametemebea katika wilaya hiyo na kujionea maeneo ya viwanda hivyo.
Awali kabla ya kutembea katika Kijiji cha visegese ambapo kuna viwanja ya maeneo ya uwekezaji mkuu wa wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu ambaye
ni mwenyeketi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo
aliwakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikisha mazingira ya usalama kwa
ajili uwekezaji
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
Mwanamvua Mrindoka amekishukuru kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kuwaleta wawekeza hao ili kufanikisha wananchi wa wilaya hiyo wanakuwa na uchumi wa kati na kuongeza kodi kwa serikali.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Brendan Maro alisema wilaya hiyo imepiga
hatua katika kutenga maeneo ya viwanja kwa ajili ya uwekezaji hivyo kwa
sasa kituo hicho hakinabudi kupeleka wawekezaji katika maeneo ya
pembezo.
Katika
mradi huo wa viwanja 291 ambao asilimi 63 ni kwa ajili ya wananchi na
asiliami 37 ni kwa ajili ya halamshauri ya wilaya ya Kisarawe na wabia
wa mnradi huo kwa mafanikio hayo uwe ni chachu kwa halmashuri zingine ili kukuza uchumi kwa wananchi kwa kutenga maeneo ya viwanda na kupima hali itakayosaidia kuepukana na mipango miji holela.
0 comments:
Post a Comment