Home » » AZAM FC WAANZA MAJIGAMBO

AZAM FC WAANZA MAJIGAMBO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 

UONGOZI wa timu ya Azam FC umetamba kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ili waweze kutetea ubingwa wao.

Azam FC kwa sasa wapo kileleni baada ya kujikusania pointi sita sawa na Mtibwa Sugar zote zikiwa zimecheza kila moja mechi mbili.

Akizungumza Dar es Salaam juzi,Meneja wa Azam FC Jemedari Said alisema kuwa wanajivunia sana kwa kufanya usajiri wa maana na hivyo kuwawezesha kushinda kila mechi akiwemo Mrundi Didier Kavumbagu ambaye alitokea Yanga.

"Kwa sasa Kavumbagu amekuwa ni msaada tangu kuanza kwa ligi ni shambuliaji anayepanda na kushuka anauwezo mkubwa sana,"alisema.

Jemedari alisema kuwa kazi kubwa inafanywa na Kipre Tchetche ambaye anamsaidia sana Kavumbagu, ambapo timu inacheza kama timu na kwa sasa si jambo la kushangaza kwa wadau kuona Azam inakuwa kileleni .

Meneja huyo aliongeza kuwa timu ipo katika maandalizi mazuri   kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa ugenini dhidi ya wenyeji Prisons utakaofanyika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Jumamisu ijayo.

Katika hatua nyingine Meneja huyo wa Azam FC, alisema kwamba beki wao David Mwantika na kiungo Kelvin Friday hawatasafiri kwa sababu ni majeruhi.

Mwantika anaelezwa kuwa aliumia kifundo cha mguu katika mechi na Ruvu Shooting, wakati Friday anasumbuliwa na maumivu ya misuli ambapo wote watakuwa nje kwa wiki moja .

"Tuna matumaini kwamba tukitoka Mbeya majeruhi watakuwa na nafuu kwa kuwa wapo kwenye matibabu na wataanza mapema mazoezi mepesi mepesi," alisema.

Pia Azam FC itawakosa Nahodha wake, John Bocco ‘Adebayor’, Frank Domayo, Joseph Kimwaga na Leonel Saint Preux, ambao wote ni majeruhi pia

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa