Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VITENDO vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake vimekithiri
wilayani Mkuranga mkoani Pwani hatua inayopelekea asasi ya kiraia kutoa
elimu ili kupunguza tatizo hilo.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi mjini Kibaha, Mratibu wa Asasi
isiyo ya kiserikali ya Kibaha Palarigo Centre (KPC) Mohamed Kiaratu
alisema, matukio zaidiu ya kumi yametokea katika wilaya hiyo katika
kipindi cha miezi tisa.
Alisema kuwa matukio hayo ni pamoja na ubakaji wa watoto, wanawake
kuuawa kwa wivu wa mapenzi na uvamizi wa kituo cha polisi
kulikosababisha kifo cha askari.
Kiaratu alisema, wanatafuta fedha ili kuweka kambi katika wilaya hiyo
na kuweza kutoa elimu ili kutokomeza vitendo hivyo katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa kwasasa asasi hiyo inaendesha mafunzo ya siku tatu ya
kuelezea ukatili wa kijinsia, kwa washiriki 40 wanaotoka katika
Halmashauri ya wilaya ya Kibaha mjini na Vijijini.
Alisema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa KPC na
Jumuiya ya kitengo cha jamii cha sheria kupinga unyanyasaji wa kijinsia
kwa ufadhili wa fedha kutoka serikali kuu wizara ya katiba na sheria.
Alisema kuwa asasi hiyo ilianzishwa mwaka 1999 ikiwa na wanachama 24
ambapo kwa sasa ina wanachama 120, ikiwa na malengo ya kutoa elimu ya
utetezi wa wanawake na watoto kwa haki za binadamu.
Chanzo:Tanzani Daima
0 comments:
Post a Comment