Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI wametakiwa kuachana na tabia ya kubadilisha viongozi kama mashati, hata pale inapobainika kuwa ni kiongozi mtendaji.
Wito huo ulitolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Abdulrahaman Kinana, wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ofisi ya CCM
wilaya ya Kibaha.
Kinana alisema, hakuna haja ya kuendelea kubadilisha viongozi kama
mashati, iwapo wapo wanaoletea mabadiliko kwenye jamii na chama kwa
ujumla.
Alimpongeza mbunge wa jimbo hilo Silvestry Koka kwa uamuzi wa kujitolea kujenga ofisi ya chama hicho.
Kinana alisema, wapo watu wengi wana fedha zao lakini hakuna wanachokifanya kwenye chama na jamii wanayoiongoza.
"Kwenye chama anapopatikana kiongozi kama Koka ni kitu cha kujivunia tunatakiwa kumpa ushirikiano ili chama kiendelee"alisema.
Kinana yuko katika ziara kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama na miradi mbalimbali katika mkoa huo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment