Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHIRIKA
la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), limesema mgodi wa kufua umeme
uliojengwa Kidatu Morogoro mwaka 1975, bado una uwezo wa kuzalisha
nishati hiyo kwa kiwango cha kutosha.
Kauli hiyo, ilitolewa juzi na Meneja wa Mgodi huo, Injinia Joseph
Lyaruu, wakati wa ziara ya wandishi wa habari nchini, kujionea kazi
zinavyofanyika katika mgodi huo.
Alisema uwezo huo ulitokana na jitihada za Tanesco kuendelea
kuuboresha hatua kwa hatua, ambako hivi sasa katika mgodi huo kumefugwa
mashine nne ikilinganishwa na awamu ya kwanza ulipojengwa, ambazo zina
uwezo wa kuzalisha umema kwa ufanisi mkubwa ambao unakwenda sambamba na
ongezeko la wateja kila mwaka.
“Sio kweli kama mtambo hauwezi kuzalisha umeme kama inavyodhaniwa na
baadhi ya watu, bado unao uwezo wa kufanya kazi katika kipindi cha miaka
50, hata nchini India iko mitambo ambayo imefanya kazi zaidi ya miaka
50,” alisema Injinia Lyaruu.
Lyaruu, alisema Watanzania hawana haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu
uzalishaji katika mgodi huo, kwa sababu shirika kwa kushirikiana na
wahisani wako katika mkakati kubadili baadhi ya vifaa ambavyo vimekuwepo
tangu unajengwa.
Akizungumzia kuhusu hali ya maji, Lyaruu alisema Watanzania watarajie
kupata huduma hiyo kwa ufanisi na bila kikomo, kwa sababu kipindi hiki
maji ya kutosha yapo.
Alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni uhaba wa maji,
shughuli za kibinadamu karibu na mito inayoingia kwenye mabwawa na
uchepushaji wa maji kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu, Rashid Msingwa, alisema
mgodi huo una wafanyakazi 104, ambao wanafanya kazi mbalimbali ikiwemo
utoaji wa huduma za jamii.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment