Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFANYABIASHARA wa mazao ya misitu wilayani Kisarawe, Pwani
wameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Misitu Nchini
(TFS) kumwondoa ofisa wake, Mathew Mwanuo na kuwaletea mwingine.
Mwanuo anatuhumiwa na wafanyabiashara hao kuwalazimisha watoe rushwa
kila wanapokwenda msituni kuvuna mkaa na mazao mengine yatokanayo na
misitu.
Akisoma maazimio ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wao juzi, Katibu
wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Mazao ya Misitu (Uwamami), Ally Kombo,
alisema wanaitaka TFS imwondoe ofisa huyo.
Kombo alitaja sababu kubwa ya kutaka aondolewe ni kukosa imani na
utendaji wa Mwanuo wa kulazimisha rushwa kwa kutafuta makosa ya uongo,
ili apate chochote.
“Wafanyabiashara wenzangu baada ya kuwasikiliza kwa kina, niliwahoji
kama mnataka tuendelee na hadha hii… wengi mlisema mnataka Mwanuo
aondoke Kisarawe, hivyo tunaiomba TFS imwondoe ofisa huyo,” alisema.
Wafanyabiashara hao pia wamewataka maofisa wa Mamlaka ya Mapato
Nchini (TRA) na Askari wa Jeshi la Polisi wanaopangiwa katika vizuizi
viwili Pugu Kajungeni na Mwisho wa Lami kufuata sheria ya kazi na siyo
kulazimisha makosa ili waandike faini.
Akizunguma na Tanzania Daima kuhusu tuhuma hizo, Mwanuo alisema si
kweli na kwamba atayashughulikia malalamiko hayo kwa kukaa na viongozi
wa wafanyabiashara hao pindi atakaporejea kutoka likizo.
“Yaliyoelezwa na wafanyabiashara hao si ya kweli, ni uzushi mtupu…
nipo likizo na ninatarajia kurejea ofisini Julai 17 mwaka huu, nikirudi
tu nitawaomba viongozi tuzungumze,” alisema Mwanuo.
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFS, Bakari Mohamed, alisema ofisi
yake haijapelekewa malalamiko yoyote na kwamba atatafuta nafasi ya
kukaa na wafanyabiashara wote waeleze tatizo lilipo, ili walimalize
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment