Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu 11 wanaodaiwa kuwa
raia wa Ethiophia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sharia.
Waethiophia hao walikamatwa juzi, saa tisa usiku, katika kijiji cha Ukuni kata ya Dunda, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei,alithibitisha kukamatwa
raia hao na kusema walikamatwa wakiwa wamejificha vichakani karibu na
barabarani wakisubiri usafiri wakuondoka.
Kamanda Matei alisema raia hao wanadaiwa kuingia katika mkoa huo kwa
kupitia njia za baharini ambapo hadi sasa haijajulikana walikokua
wakielekea huku wote wakiwa hawana vibali.
Aliwataja watu hao kuwa ni Amoree Achem (22),Worko Hule (26) Basiad
Tekiara (38) Anamaiyo Ramri (21), Fekri Angole (23) Kassa Dewenj
(28),Wengine ni Antiosogaso Suraj (20) Abara Charkiso (30), Mmbarak
Diljigab (30), Nichacho Abiche (32) na Kafasa Serecho (40).
Watuhumiwa watakabidhiwa idara ya Uhamiaji kwa taratibu nyingine
Chanzo;Tanzani Daima
0 comments:
Post a Comment