Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya wakazi 300 wa mitaa ya Viziwaziwa, Mikongeni na Sagale,
wilayani Kibaha, wameazimia kugawana shamba la 117, mali ya Saeni
ambaye amelitelekeza kwa zaidi ya miaka 22 sasa.
Shamba hilo ambalo lipo katika mitaa hiyo limekuwa chanzo cha
wanafunzi wengi kukatisha masomo kutokana na kufanyiwa vitendo vya
ubakaji na hatimaye kupata mimba, huku vitendo vya mauaji na uporaji
vikifanyika katika eneo hilo ambalo limekuwa na pori kubwa.
Wakizungumza kwenye mkutano wa pamoja wakazi wa vijiji hivyo chini ya
uongozi wa muda wa Mwenyekiti Shabani Matimbwa, walisema wamekuwa
wakijadili changamoto hiyo kwenye mikutano halali ya mitaa yao, lakini
viongozi waliopo madarakani hawachukulii uzito suala hilo wala
kulitolea majibu kwenye mikutano.
Akizungumza kwenye mkutano huo ambao uliwashirikisha wananchi wa
mitaa hiyo waliounda umoja wao wa mitaa hiyo ‘Vimisa’, mwenyekiti
huyo wa muda alisema walikubaliana kuwaita Diwani wa Kongowe, Salum
Bagumeshi, mwenyekiti wa mitaa hiyo, mtendaji na kiongozi wa polisi
kata, ili kufikia muafaka wa kuligawa shamba hili na kujenga shule ya
sekondari, upanuzi wa zahanati, soko pamoja na kutenga eneo la kiwanja
cha michezo.
Wananchi hao walikubaliana kutenga ekari 30 kwa ajili ya mambo ya
maendeleo, na ekari zilizobakia kugawana kila mmoja aliye ndani ya
‘Vimisa’ aweze kupata eneo la kulima na wengine kujenga kwa maendeleo
yao.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment